Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Mh. Ridhiwani Kikwete, akizungumza wakati wa kukabidhi Saruji mifuko 20 kwaajili ya uanzishwaji wa shule ya Msingi Kitongoji cha Choza.
....................................
Na
Shushu Joel, Chalinze.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Mh. Ridhiwani Kikwete amekabidhi msaada
wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi
wa shule ya Msingi katika kitongoji cha Choza, Matofali Elfu tatu, fimbo nne
maalum kwa ajili ya walemavu wa macho, Kadi 23 za Afya kwa ajili ya matibabu ya
wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi Milioni tano.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa kata, vijiji na
vitongoji wa kata hiyo alisema kuwa amefanya maamuzi hayo ya kuanzisha ujenzi
wa shule hiyo kutokana na changamoto zinazowakabili wazazi/walezi na wanafunzi
kwa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata elimu ya shule ya msingi huku
wazazi kwa ajili ya masuala ya kimaendeleo.
Aliongeza kuwa kuongezeka kwa watu
katika eneo hilo la choza kumepelekea kuhitajika kwa haraka kwa huduma za
kijamii ili kuendana na mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.
"Saruji niliyotoa
ni uanzilishaji wa ujenzi wa shule hiyo lakini si kwamba ndio mwisho wa utoaji
wangu wa mahitaji katika ujenzi huo bali ni kama kiongozi wa mfano ili hata
wananchi wanapoambiwa wachangie wasisite" Alisema Ridhiwani Kikwete.
Aidha
aliongeza kuwa wananchi ndio nguzo ya maendeleo hivyo wanapoamua jambo lolote
lile la kimaendeleo ni lazima lifanyike kutokana na umoja, nguvu na mshikamano
wao katika ufanikishaji wa maendeleo katika eneo husika.
Mara baada kutoa
saruji hiyo Ridhiwani aliwataka viongozi wa eneo hilo kutafuta eneo lingine
kubwa lenye kufaa ujenzi wa zahanati ili pia choza pajengwe zahanati.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa choza kujitokeza kwa wingi katika kuhamasishana juu ya
maendeleo kwani serikali inatambua makusudi yao.
Kuhusu
misaada aliyoitoa, Mh Mbunge alisema kuwa ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa
ahadi za Ilani ya Uchaguzi na maombi mbalimbali ya wananchi.Katika shughuli hiyo
pia Mhe.Mbunge alikutana na wanachama mbalimbali wa vikundi vya Maendeleo
katika kata hiyo .
Kwa upande wake diwani wa kata
hiyo ya ubena zomozi Nicholaus Muyuwa amempongeza Mbunge huyo kwa uanzilishi
wake wa kutoa saruji kwa lengo la ujenzi wa shule katika eneo hilo ili
kuwaondolea changamoto watoto wa maeneo hayo.
Aidha amemhakikishia Ridhiwani
kuwa mifuko hiyo itatumika kama ilivyokusudiwa kufanyika kwani hata wao
walikuwa wakilifikiria tu lakini Mbunge wetu kafanya kweli juu ya hilo hivyo
utoaji wake wa hiyo mifuko kwa wananchi kweli Ridhiwani Kikwete ni kiongozi wa
mfano.
Naye Cosmos Alphonce ni Mwenyekiti wa kijiji cha kaloleni ameshukuru kwa
mchango uliotolewa na Mbunge na kumtaka aendelee na moyo huo wa kujitolea kwa
wananchi wake.
Aliongeza kuwa kujengwa kwa shule katika eneo hilo kutaondoa
changamoto ya watoto wa eneo hilo kutembea kilometa nyingi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Mh. Ridhiwani Kikwete, akiwakabidhi fimbo maalum za kuwaongoza kutembea walemavu wa kata ya Ubena.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi msaada wa Baiskeli ya
Miguu mitatu (Wheel Chair), Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe
ambaye ni mlemavu wa miguu.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Mh. Ridhiwani Kikwete, akiwa anarekebisha Baiskeli inayomsadia kutembea mlemavu wa miguu Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe wakati alipokabidhi vifaa mbalimbali kwa walemavu wa kata ya Ubena.
No comments:
Post a Comment