Mwenyekiti
wa Taasisi ya Adullah Aid Tanzania, Arif Yusuf
..........................................
Na
Shushu Joel,chalinze.
TAASISI ya Miraj Islamic Centre yenye makao yake mkuu
jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa watu wote walio na nafasi ya kipato kuweza
kuwasaidia wasio na kipato kama ilivyoagizwa katika vitabu vya Mungu.
Rai hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Arif Yusuf Abdulrehman maarufu
Arif Tanzania alipokuwa akizungumza na baadhi ya waislamu wakati wa zoezi la
kugawa futari kwa wakazi wa vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Arif, alisema kuwa Taasisi yake imekuwa miongoni mwa taasisi za kuigwa ndani na nje
ya Tanzania kwa jinsi inavyojitolea kuwasaidia watanzania wote bila ya kujali dini zao wala
kabila huku lengo likiwa ni kuwaonyesha wale wasio na uwezo kuona ni sawa na
wenye uwezo.
"Unaposaidia wenzako Mwenyezi Mungu anakuongezea kutokana
na jinsi wale unaowasaidia wanavyokuombea uweze kupata ili uendelee kuwasaidia
zaidi"Alisema Arif Tanzania.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki cha mwezi huu
wa Ramadhani taasisi ya Miraj Islamic imewezesha sehemu mbalimbali kwa ajili
wananchi vyakula na tende kwa baadhi ya mikoa kama vile
Arusha, Pwani, Mwanza, Kigoma, Zanzibar na Mikoa mingine kwa kusudi la kuwasaidia
wasio na uwezo wala kipato ila wanafunga Ramadhani.
Aidha alisema kuwa Taasisi
yake imekuwa msaada mkubwa kwa serikali kutokana na jinsi inavyojitoa katika
masuala ya kusaidia watu mbalimbali ili waweze kujikwamua katika maisha
yao, watu hao ni pamoja na kuwasaidia usafiri walemavu, vijana kuwapatia mashine
za kukamulia juice na wengine kuwapatia pikipiki kwa ajili ya kufanya shughuli
za boda boda, kinamama kuwawezesha kwa Vyerehani ya ushonaji.
Hivyo kama kila
mwenye nafasi ya kipato akijitolea kwa moyo mmoja basi watakuwa wamewafikia
watanzania wengi na kuwawezesha ili nao waondokane na umasikini walionao.
Pia
Arif Tanzania ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt
John Magufuli kwa jinsi inavyofanya kazi zake na Viongozi wa Dini zote na
kuwakomboa watanzania wa hali za chini.
Kwa upande wake Ashura Juma (81) mkazi
wa vikindu katika wilaya ya mkuranga mkoani Pwani ameipongeza taasisi ya Miraj
Islamic Centre kwa jinsi inavyojitolea katika kutoa misaada mbalimbali kwa
wanyonge.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kupitia taasisi hiyo familia yake imekuwa moja ya wanufaikaji wakubwa
kwa kupata misaada mingi ikiwemo Chakula kwa ajili ya futari, fedha na mahitaji
mengine mengi ya kibinadamu.
Aidha Mama huyo amemtaka Mwenyekiti wa taasisi
hiyo Arif Tanzania kuendelea na tabia hiyo ya kujitolea kwani wanufaika wako
wengi na wataendelea kumuombea ili aweze kupata.
Akizungumza kwa niaba ya
wananchi wa halmashauri ya chalinze katika wilaya ya bagamoyo, Mbunge wa jimbo
hilo Ridhiwani Kikwete amesema kuwa misaada hiyo inayotolewa na taasisi hiyo
imekuwa na tija kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu kutokana na uhitaji wa
futari kwenye kipindi hiki.
Mbali na hilo Kikwete alisema kuwa pongezi hizo si
kwa wananchi bali hata serikali imekuwa ikinufaika na Arif Tanzania kupitia
taasisi zake zinazojitolea kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya wanyonge.
"Kutokana na jinsi taasisi hii inavyojitolea katika ufanikishaji wa wa
misaada ni lazima sie kama wawakilishi tuisemee vizuri ili wengine wajitokezw
"alisema
No comments:
Post a Comment