NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Jeshi
la kujenga Taifa (JKT) kuongeza nguvu ya ukarabati wa Uwanja wa mpira wa Miguu
wa Ilulu Stadium uliopo Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi.
Uwanja
huo wa Ilulu unatarajiwa kutumika katika fainali za Azam Federation Cup (FA)
Zitakazofanyika Juni mosi mwaka huu 2019.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Mkuu wa Wilaya ya Lindi ambae pia ni mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya uwanja huo Shaibu Ndemanga alisema kuwa wanajeshi hao
wameshaanza kuwasili toka siku ya Ijumaa ya tarehe 10 mwezi huu na wataanza
kufanya kazi hiyo mapema juma tatu ya Mei 13.
Alisema
mpaka sasa tayari wanajeshi 13 wameshawasili na wanatarajia kuwa na wanajeshi
30 ambao watashiriki katika kukarabati uwanja huo huku akitaja fani za
wanajeshi watakaofanya kazi hizo kuwa ni pamoja na Wahandisi wa Ujenzi, mafundi
ujenzi pamoja na wataalamu wa ujenzi.
Ndemanga
pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa
kukubali ombi lao la kuwatumia wanajeshi hao katika shughuli za ukarabati wa
uwanja huo
No comments:
Post a Comment