Friday, May 10, 2019

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
(UNICEF) Tanzania, Bi. Maniza Zaman (kushoto) alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mei 10, 2019 Jijini Dodoma, katikati ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Bi. Maniza Zaman, (kushoto) akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kulia ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusu ushirikiano baina ya UNICEF na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy).

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akionyeshwa picha ya Watoto na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment