NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Serikali
imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuweka umeme
katika taasisi za umma vijijini ambako miradi ya umeme vijijini REA inapita.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Nishati Dkt Medardi Kalemani jana mei 20 alipokuwa
anazungumza na wakazi wa kata ya Namangale katiaka Halmashauri ya Wilaya ya
Lindi Mkoani humo katika hafla fupi ya uwashwaji wa Umeme katika shule ya Msingi
namangale kijijini hapo.
Kalemani
alisema kama serikali ilipoamua kuanzisha mradi huo wa umeme vijijini REA moja
ya Vipaumbele vyake ni kuwekwa katika Taasisi za Umma ambako kwa kiasi kikubwa
wananchi wanakwenda kupata huduma katika maeneo hayo.
Alisema
ni vyema viongozi hao wakajiwekea utaratibu wa kutenga fedha kwa ajili ya
maeneo hayo mapema iwezekanavyo kwani Serikali itaanza kufanya Ziara maalumu ya
kukagua majengo hayo ili kuhakikisha kila kijiji ambacho kimepitiwa na mradi
huo taasisi zake zimewekewa umeme.
“Kwahivyo
wenyeviti wa vijiji, madiwani pamoja na Wakurugenzi tengeni fedha mahususi
kabisa kwa ajili ya kupeleka katika Mashule, Zahanati, Vituo vya Afya pamoja na
miradi ya maji kote humo lazima kuwekewe umeme kwa kuwa wananchi ndiko
wanakokwenda kupata huduma” alisema Waziri Kalemani Kalemani.
Aliongeza
kuwa Inasikitisha kuona umeme umefika kijijini lakini wakati unatembelea
utashangaa kuona wananchi wananyoosha mikono wanakuambia eti wao kituo chao cha
Afya hakina Umeme cha kushangaza unamuuliza mwenyekiti wa kijiji kama
ameshalipia umeme kwa ajili ya kuunganishiwa lakini anakosa majibu.
Katika
kuunga Mkono jitihada hizo za Serikali Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya State grid
inayotekeleza mradi wa REA Vijijini katika Mkoa wa Lindi Charles Mlawa alihaidi
kuweka mfumo wa Umeme katika Shule ya Msingi ya Namangale iliyopo katika kata
ya Namangale Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ili kuifanya shule hiyo kuwa na
umeme wa kutosha na wa uhakika
No comments:
Post a Comment