Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy, kushoto, na kulia ni Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamedi Usinga
.................................
Ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri
ya Bagamoyo umeongezeka mara kumi
zaidi ukilinganisha na siku za
nyuma.
Hayo yamebaishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Aliy Aliy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi
wa Halmashauri mara baada ya kumaliza kikao cha baraza la madiwani
kilichomalizika leo.
Mwenyeki huyo wa Halmashauri alisema kuwa
Halmashauri ya Bagamoyo imejipanga vizuri katika vyanzo vyake vya mapato ili
kukusanya mapoto halisi yanayo kusudiwa
na kufikia lengo lililowekwa na Halmashauri katika kukusanya
mapato ya ndani.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo
unategemea ukusanyaji mzuri wa mapato ambapo kwa namna walivyojipanga wameweza
kukusanya mapato mara kumi
zaidi ya kawaida.
Akivitaja vyanzo vya mapato ambavyo wameweza kuvisimamia vizuri ni
pamoja na Kituo cha mabasi, Geti la kukusanya
ushuru kwa maliasili sanzale, Ushuru wa samaki pamoja na machimbo
ya Mchanga yaliyo eneo la Kiromo ambapo
hivi karibuni wanatarajia kupeleka nguvu
zaidi kwenye ukusanyaji kodi zamajengo.
Kufuatia Hali hiyo, Mwenyekiti huyo ambae ni
Diwani wa kata ya Fukayosi, alisema ana matumaini makubwa kwamba wanaweza
kufikia lengo la kukusanya bilioni 2 na
milioni mia nane ili kukidhi mahitaji ya
Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Aliongeza kuwa, katika mikakati ya kuhakikisha
halmashauri inakusanya mapato ya
kutosha, imeongeza kodi za pango kwa watumishi wanaoishi kwenye nyumba za
serikali na kwamba tayari watumishi wa serikali wamepewa mikataba mipya
kwaajili ya ongezeko la kodi ya pango.
Aidha, aliongeza kuwa, katika makusanyo hayo
asilimia kumi inarudishwa kwenye kata zinazosimamia makusanyo hayo ili kata nazo zifanye
maendeleo yake ya kata ambapo hiyo itakuwa ni motisha kwa kata kuendelea kukusanya mapato kwa wingi.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Halmashauri
alisema kuwa, licha ya kasi ya ukusanyajiwa
mapato lakini bado wanaendelea
kumthamini mwananchi wa kawaida wa chini anaefanya biashara ndog ndogo.
Alisema kwa wafanyabiashara ndogondogo ambao
hawapo kwenye fremu hawatalipa kodi kama
alivyoagiza Rais wa Jamhuriya Muungano,
vinginevyomtu awe ameweka biashara yake kwenye fremu.
Alitolea mfano wa wauzaji mkaa wa majumbani
hawatalipa ushuru mpaka wawe kwenye
fremu na wakaanga chipsi wa mitaani pia
hawatalipa ushuru vinginevyo awe anakaangia ndani ya fremu