Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwani Athuman akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) jijiji Dar es Salaam leo, kuhusu Jeshi la Polisi
kutokubali kuona kundi la watu wachache linatishia usalama wa maisha ya raia na
mali zao, Wote watakaobainika kuwa ni wahalifu watakamatwa na kuchukuliwa hatua
za kisheria.
JESHI la
Polisi nchini kwa kishirikiana na Ofisi za Interpol Kanda ya Kusini Mwa
Afrika imefanya operesheni na kukamata vipande vya meno ya Tembo 666
vyenye uzito wa Kilogram 1279.19 vyenye thamani zaidi ya a Sh. Biloni Nne.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa
Jeshi la Polisi (CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa vipande hivyo vya
tembo yamehusisha watu tisa kati yao mmoja ni Raia wa Guinea na mwingine
ni Raia wa Uganda.
Amesema kuwa
katika operesheni Usalama III wameweza kukamata vitu mbalimbali
kutokana na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati wa matayarisho ya
operesheni ya Usalama III, ambapo waliweza kukamata mitambo ya 18 ya
kutengenezea gongo pamoja na lita za gongo 960
zimekamatwa.
Athuman
amesema katika Operesheni hiyo wameweza kukamata watuhumiwa 265
ambapo baada ya uchunguzi wataobainika kuhusika na vitendo
vya kihalifu watafikishwa mahakamani mara moja ikiwa namna au nyingine katika
kufankisha vitendo vya kihalifu.
Kamishina
Othman amesema ametoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi kuwasiliana na
ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi magari yanakotoka kwa uchunguzi kabla
ya kuyanunua ili kuondoa usumbufu wa kukamatwa mara kwa mara katika operesheni
kama hizi.
Amesema
kutokana na operesheni hiyo jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la watu
wachache linalotishia usalama maisha raia wema na mali zao na
wataobainika kufanya hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria bila kusita.
No comments:
Post a Comment