Mkuu wa Wilaya ya
Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum(watatu kushoto) akikata utepe
kuashiria kupokea kwa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation
kwa ajili ya shule 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani.Hafla hiyo ilifanyika
katika Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani jijini.Kutoka
kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Janester Emily,Kaimu Afisa elimu shule za
msingi kinondoni,Chitegese Dominic, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano
wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania
Foundation,Renatus Rwehikiza.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ally Salum akimsalimia mwanafunzi wa darasa la
nne katika shule ya msingi Mchangani iliyopo Mwananyamala Kisiwani jijini,
Hashim Jumanne baada ya kupokea msaada wa madawati 500 kwa niaba ya shule za 5
za kata ya Mwananyamala Kisiwani yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation
jana.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum akiongea na wanafunzi pamoja na
Uongozi wa Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani, wakati wa
hafla ya kupokea msaada wa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania
Foundation kwa ajili ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani,Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza.
No comments:
Post a Comment