Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
Habari kuhusu matokeo ya kidato cha sita 2016.
Ufaulu wa kidato cha sita 2016 umeonekana kushuka kwa asilimia 0.93 baada
ya ufaulu wa jumla kuwa asilimia 97.94 ukilinganisa na mwaka 2015 ambao ulikuwa
asilimia 98.87.
Hayo yalibainishwa leo jijini Dar es Salaam, na Katibu mtendaji wa
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde, alipokuwa
akitangaza matokeo ya kidato cha sita 2016 mbele ya waandishi wa Habari.
Dkt. Msonde alisema Ufaulu wa jumla katika Mtihani wa Kidato cha Sita
2016 unaonesha kushuka kwa asilimia 0.93
ambapo mwaka 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 98.87 na mwaka 2016 ufaulu ni asilimia 97.94.
Hata hivyo, ubora wa ufaulu umeonekana kuimarika kwa kuwa idadi ya
watahiniwa waliofaulu vizuri katika daraja la I, II na III imeongezeka kwa
asilimia 3.72 kutoka asilimia 89.41 mwaka 2015 na kuwa asilimia 93.13 mwaka 2016.
Alisema Jumla ya watahiniwa 74,896
waliandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2016 wakiwemo
wasichana 27,717 (37.01%) na
wavulana 47,179 (62.99%) ambapo
kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa Shule walikuwa 65,585 na watahiniwa wakujitegemea
walikuwa ni 9,311.
Aidha, alisema kuwa, kati ya watahiniwa 74,896 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei 2016,
watahiniwa 73,940 sawa na
asilimia 98.72 walifanya mtihani
na watahiniwa 956 sawa na
asilimia 1.28 hawakufanya
mtihani.
Aliongeza kuwa, Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 63,528 sawa na asilimia 97.94 ya waliofanya mtihani huku wasichana
waliofaulu ni 24,062 sawa na
asilimia 98.59 na wavulana ni 39,466 sawa na asilimia 97.55. 3 ambapo Mwaka
2015 Watahiniwa 34,777 sawa na
asilimia 98.87 ya Watahiniwa wa
Shule walifaulu mtihani huo.
Dkt. Msonde alisema takwimu za ufaulu kimasomo zinaonesha
kushuka kwa ufaulu, katika masomo ya Sayansi
kati ya asilimia 5.36 na 8.9; masomo ya Sanaa kati ya asilimia 0.00
na 4.43 na masomo ya Biashara kati ya asilimia 1.7 na 6.9.
|
No comments:
Post a Comment