Moto ukiendelea kuwaka katika moja ya majengo ya Shule hiyo.
Mpaka moto huu ulipodhibitiwa mali zifuatazo zilikuwa tayari zimeshaungua:-
•
Madarasa tisa yameungua, ambapo matano yameungua pamoja na samani
zilizokuwa ndani na mengine manne ni majengo peke yake Vifaa viliwahi
kuokolewa na wananchi.
• Ofisi nne za walimu.
• Maabara mbili za kemia na fizikia zimeungua kwenye paa tu, hivyo samani za ndani hazijaungua.
• Takribani madawati zaidi ya 300 yameteketea kwa moto.
Majengo mengine ya shule yapo salama yakiwemo mabweni.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amewaomba wananchi na uongozi wa
shule kuwa watulivu wakati Uongozi wa Mkoa Ukitafuta namna ya Kusaidia
Wanafunzi Kuendelea na Mafunzo baada ya kufunguliwa kwa Shule hiyo kesho
Julai 11, 2016
Aidha,
Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kuuzima moto huo
kwani haikuwa kazi rahisi, pia amewashukuru Polisi na Jeshi la zimamoto
kwa jitihada walizochukua katika kuudhibiti moto huo.
Kwa
sasa inafanyika tathmini ya mali zilizoteketea kutokana na moto huo
sambamba na uchunguzi wa chanzo cha moto. Taarifa kamili ya uchunguzi na
tathmini itatolewa pindi itakapokamilika.
Katika
hatua nyingine mtu mmoja alietaka kuiba Komputa mpakato katika tukio
hilo amekamtwa na Polisi Baada ya Wananchi kuanza kumpa adhabu.
Haya majanga ya moto sasa nadhani ifike wakati kuwekwe na mkakati maalumu kbaini haswa chanzo chake kwani yanashika kasi kila kukicha.
ReplyDelete