Tuesday, July 26, 2016

DC BAGAMOYO AKABIDHI MADAWATI KWA MKUU WA MKOA.

Mkuu wa Mkoa wa  Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo wa tatu kutoka kushoto, akijaribu  Madawati wilayani Bagamoyo,wa kwanza  kulia nimkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga, na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa jimbo la  Bagamoyo, Mh. Shukuru  Jumanne Kawambwa, wa pili kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa Sayona Group, Aboubakari Mlawa.


Mkuu  wa wilaya ya Bagamoyo  Majid Hemed Mwanga, amekabidhi madawati kwa mkuu wa mkoa Pwani, na kufanikiwa kumaliza tatizo la  madawati  kwa wilaya  ya Bagamoyo.

Akisoma taarifa ya  utekelezaji wa agizo la Rais la kutengeneza madawati,  ambalo limesimamiwa na mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alisema wilaya yake, imekamilisha mahitaji yote ya madawati  kwa shule za msingi na sekondari.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo alisema madawati yote hayo  yametengenezwa kwa msaada kutoka kwa wadau mbalimbali na hivyo kuokoa fedha za serikali zaidi ya milioni mia  tano ambazo  zingetumika  kutengeneza madawati  hayo.

Aliongeza kwa kusema jamii imejitolea kusaidia kwa namna mbalimbali kufanikisha zoezi hilo la utengenezaji  wa madawati ambapo alitumia  nafasi hiyo kuwashukuru wadau wote waliochangia upatikanaji wa madawati hayo akiwemo Shubashi Pateli ambae amechaniga madawti 1,200, na Mwenyekit wa makampuni ya IPP Reginald Mengi akiwa aliyechangia madawati 500.

Mkuu huyo wa wilaya  alisema wilaya imeandaa mikataba ya kuyatunza madawati hayo na kwamba mwalimu au mtumishi yeyote  atakaechangia uharibifu wa madawati hayo hatua zitachukuliwa dhidi yake.

Alisema wilaya imejiwekea mikakati ya kuhakikisha uhaba wa madawati hautokei tena  ili kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa chini katika kipindi ambacho Rais ametangaza elimu bure kwa wote

Mkuu wa mkoa wa Pwani  akielezea jambo wakati akikagua Madawati, kulia  ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy  Issa.

Aikpokea taarifa hiyo ya madawati, mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist  Ndikilo, ameipongeza wilaya ya  Bagamoyo kwa kukamilisha utengenezaji wa madawati, na kuongeza kuwa mkoa wa Pwani umefanikiwa kutengeneza  madawati ya  sekondari kwa asilimia 100.4 huku yale ya  shule za msingi ni asilimia 93 ambapo asilimia saba iliyobaki yanaendelea kutengemnezwa.
 



Haya ni baadhiya madawati yaliyotengenezwa wilayani Bagamoyo
Diwani  wa kata ya Dunda kushoto, Dikson  Makamba akipokea madawati kutoka kwa mkuu wa mkoa, kwaajili ya kata yake
Kutoka kushoto ni Mh.Togo Omari, Diwani viti maalum Yombo,  wa  pili  kutoka kushoto ni Mh. Subira Mgalu, Mbunge  viti maalum  Pwani, wa tatu ni Mh. Shumina Ismail Rashid, Diwani viti maalum Mwambao, wa nne ni Mh. Hafsa Juma Kilingo Diwani viti maalum Mwambao, na wa kwanza kulia ni Rehema Mwene, Diwani kata ya Lugoba. wakijaribu madawati katika ofisi ya mkuu wawilaya Bagamoyo
Diwani wa  kata  ya Mapinga,  Ibrahim Mbonde akipokea madawati kwaajili ya kata yake.
Diwani wa kata ya Nianjema, akipokea madawati kwaajili ya kata yake.

1 comment: