Meneja mfawidhi huduma kwa wateja, Juma Msabaha, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu huduma ya Call Center. |
Benki ya Amana imezindua huduma mpya kwa wateja
wake, kwa njia ya simu (Call Center) iliyopewa jina AMANA BANK MTAANI, lengo likiwa ni kuboresha huduma
kwa wateja wa Benki hiyo inayofuata sheria ya kiislamu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika
uzinduzi wa huduma hiyo, uliofanyika makao makuu ya benki ya Amana jijini Dar
esSalaam, Meneja Mfawidhi, huduma kwa wateja, Juma Msabaha, alisema lengo la
huduma hiyo mpya iliyopewa ni kuwasogelea wateja ili kuboresha huduma.
Alisema huduma itapatikana kwa muda wa masaa 15
kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 4 usiku ambapo katika muda huo wateja wataweza
kupiga simu na kuongea na muhudumu, anaetoa huduma kwa wateja moja kwa moja.
Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo mteja anaweza
kuuliza swali lolote linalohusu huduma za Benki ya Amana na kupata ufafanuzi bila
ya kulazimika kufika kwenye tawi Benki
ya Amana.
Aidha, Msabaha, alizitaja namba za kupiga
ilikupata huduma hiyo ni 0657980000 ambapo mawakala wa Call Center
watajibu maswali mbalimbali yanayohusu huduma za Benki ya
Amana ikiwemo aina za Akaunti za Benki ya Amana, kuhusu huduma za kibenki kwa
njia ya simu, mikopo na huduma mbalimbali.
Nae mkuu wa Kitengo cha Biashara
Munir Rajabu, alisema Benki ya
Amana imejipanga kuboresha hudama zake ambapo kwa mwaka huu wameongeza kasi ya kuwafikia wateja
kwa kuweka mawakala katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Alisema kitengo hicho cha Call Center
kitarahisisha huduma kwa wateja hasa katika maeneo ambayo Benki ya Amana haina matawi ambapo ni vigumu mteja kufika
kwenye matawi na kwa sasa mteja atapata huduma
kupitia mawakala watakaowekwa nchini kote.
Katika kipindi cha miaka mitano, Benki ya Amana
imeweza kuwa na matawi saba, ambapo
matawi matano yakiwa katika jiji laDar esSalaam, moja likiwa Arusha
na moja Mwanza, huku kauli mbiu yao ikiwa ni wateja kwanza.
Mkuu wa kitengo cha biashara Benki ya Amana, Munir Rajab akizungumzana waandishi waHabari. |
Kutoka kushoto ni meneja wa Tawi la makao makuu, Aisha Awadhi, katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Munir Rajabu, na kulia ni Meneja Mfawidhi Huduma kwa wateja, Juma Msabaha. |
No comments:
Post a Comment