Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Goodwill
Ceramic, Frank Yang (aliyeshika kipaza sauti) wakati akiangalia ramani ya
kiwanda hicho katika kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 20, kutoka kwa Balozi wa China
Nchini, Dkt. Lu Youqing (wa pili kulia) kusaidia ununuzi wa madawati katika Shule
zilizopo katika wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah
Ulega na Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa viwanda unaotekelezwa kwa kasi hapa nchini
utakuwa ndio mwarobaini wa kuondoa tatizo la ajira kwa vijana kwa wingi hapa
nakudai kuwa atakayekwamisha mkakati huo wa Serikali hatovumiliwa.
Pia amesema kuwa maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Viwanda hivyo na yale ambayo tayari ujenzi wa viwanda umeshaaza lazima miundombinu ya umeme wa uhakika upatikane ili kuwezesha viwanda hivyo kuzalisha kwa wingi.
Majaliwa aliyasema hayo juzi Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ikiwa sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi,ambapo alitembelea utekelezaji wa Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae cha Googwill,ambacho kinajengwa katika kijiji cha Kiu,kilichopo Kata ya Nyamato tarafa ya Mkamba wilayani humo.

No comments:
Post a Comment