Sunday, July 17, 2016

DC. BAGAMOYO, AREJESHA HEKA 900 KWA WANANCHI ZILIZOCHUKULIWA NA WAWEKEZAJI BILA YA KUFUATA SHERIA.

Mkuu wa wilaya  ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, (aliyesimama) akiongea na wananchi katika kijiji cha Pongwe Msungura, Kata ya Msata, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Omari Zikatimu, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Edesi Philip Lukoa, wa pili kulia ni Diwani wa Kata ya Msata, Selestin Cham Semiono.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo MajidHemed Mwanga, amerudisha heka 900 kwa wananchi, zilizokuwa zinamilikiwa na wawekezaji bila ya kufuata sheria ya umiliki Ardhi, katika kijiji cha Pongwe Msungura kata yaMsata.

Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa kijijini hapo ili kukjadili kero mbalimbaliza wananchi ikiwemo tuhuma zaubadhilifu wa fedha kwa viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho pamoja na kufanya maamuzi ya kugawa Ardhi bila ya kufikisha taarifa kwenyemkutanomkuu wa kijiji.

Majid alisema wawekezaji hao wawili ambao kila mmoja anadai  kumiliki heka 500 hali ya kuwa taratibu za kisheria hazijafutwa, huku wananchi wa kijiji cha Pongwe Msungura ambao ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa kijiji,walithibitisha kupitisha umiliki wa heka 50 tu,kama sheria inavyowataka na kwamba swalalakumiliki heka 500 kila mmoja hawalitambui.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa wilaya aliwataka wawekezaji hao kutoa maelezo namna walivyopata maeneo hayo ambapo walionyesha mihutasari ya kijiji ambayo imewapitishia kumiliki heka 500 kila mmoja.

Ili kujiridhisha na mihutasari hiyo, mkuu wa wilaya alilazimika kusoma muhutasari wa tarehe 08 julai 2013 unaodaiwa kuandaliwa na mkutano wa kijiji ili kupitisha heka 500 kwa muwekezaji ambapo aliita jina moja baada lingine ambapo wananchi  wote waliukataa muhutasari huo kwamba hawaujui.

Baada ya hali hiyo, mkuu wa wilaya aliamuru kila muwekezaji mmoja kati ya hao wawili kurudisha heka 450 na kubaki na 50 kama walivyopitishiwa na mkutano wa kijiji  na hivyo kufanikiwa kurudisha heka 900 kwa wananchi.

Aidh,baada ya kasoro mbalimbali zilizobainika katika mkutano huo, wajumbe wa Halmashauri ya kijiji walipiga kura ya kumuondoa mwenyekiti wa kijiji hicho Mbaraka Rajabu Mwelekwa,nakwamba baada ya siku 90 mkurugenzi ataitisha mkutano utakaomchagua mwenyekit mpya wakijiji cha Pongwe Msungura

Wawekezaji walionyakanywa jumla ya heka 900, kwa kuzipata bila ya kufuata sheria ya umiliki wa Ardhi vijijini, wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Pongwe Msungura kata ya Msata.
Wananchi wa kijiji cha Pongwe Msungura wakiinua mikono juu, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono maamuzi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, kuwarudishia Ardhi mikononim mwao ili ikitolewa itolewe kwa kufuata utaratibu.



Mwenyekiti wa kijiji cha Pongwe Msungura, Mbaraka Rajabu, aliyeondolewa madarakani na wajumbenwa Halmashauriya kijiji na kuungwa mkono na wananchi ambao ndio wajumbe wa mkutano mkuu, kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo,wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambae ni mkuu wa wilaya.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo,wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambae ni mkuu wa wilaya.

No comments:

Post a Comment