Sunday, July 3, 2016

DC. BAGAMOYO AFUTURISHA JANA NYUMBANI KWAKE.

Wa kwanza kulia, mwenye koti, ni mmiliki wa Blog ya bagamoyokwanza, Athumani Shomari Mkwama, akijumuika na waislamu na wananchi wengine katika futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wa pili kulia akipata futari.
wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, akijipatia futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga, nyumbani kwake.
Kutoka kushoto ni Mjumbe kutoka Zawiani Bagamoyo, Alhaji, Omari bin Yahaya bin Muhamad Raimiya, wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, walipokuwa akipata futari nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo hapo jana jumamosi.
Waislamu mjini Bagamoyo wakipata futari nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo jana siku ya jumamosi tarehe 02 Juni 2016.
Kutoka kulia ni Sheikh mkuu wilaya ya Bagamoyo, Sheikh Abdulkadiri Muhamad Ramiya, wa pili ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, wa tatu ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, anaefuata ni mjumbe wa BAKWATA wilaya ya Bagamoyo na imamu wa msikiti wa Ramia, Sheikh Simba Abubakari.

1 comment: