Mwenyekiti wa Mkutano huo, ambae ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga. |
Mkutano wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya
nne uliofanyika mjini Bagamoyo kuhusu wavamizi wa msitu wa Zigua, umetoka na
maazimio 10, ambayo yanatakiwa kutekelezwa.
Mkutano huo uliozijumuisha kamati za ulinzi na
usalama za wilaya nne ambazo ni Bagamoyo, Mvomero, Kilindi na Handeni,
umefanyika mjini Bagamoyo ili kujadili namna ya kuwaondoa wavamizi waliovamia
msitu wa Zigua.
Awali akiwasilisha mada mbele ya mkutano huo
meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania TFS
wilaya ya Bagamoyo, Charles Mwafute, alisema wameamua kushirikisha kamati za
ulinzinausalama za wilaya hizo zinazopakana na hifadhi ya msitu wa Zigua ili
kupata ushirikiano wakutosha katika kukabiliana na wavamizi.
Nae Mwenyekiti wa Mkutano huo Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga aliwataka viongozi wote katika wilaya hizo
kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa misitu ikiwa ni pamoja na kupanda miti
mipya ili jamii iendelee kuwa na misitu.
Baada ya majadiliano mkutano huo umetoka na
maazimio 10 ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa manufaa ya Taifa ili kuunusuru
msitu wa Zigua nayo ni:
1. Kuwaondoa
wavamizi wote ndani ya hifadhi ya
msitu ifikapo Tarehe 30 Septemba 2016.
2. Kila
wilaya itambue maeneo yaliyovamiwa.
3. Mtu
yeyote aliyeshiriki, au atakaeshiriki kugawa maeneo ndani ya Hifadhik
achukuliwe hatua za kisheria.
4. Kuunda
kikosi kazicha kufuatilia maeneo yaliyovamiwa na kutoa taarifa kamati.
5. Kuanzisha
Doria za mara kwa mara ndani ya hifadhi kwa wilaya zote nne mara baada ya kuwatoa wavamizi.
6. TFS,
izingatie utoaji wa motisha kwa watakaoshiriki katika doria na watakaotoa
taarifa za wavamizi.
7. Mipaka
iendelee kuimarishwa kwa kushirikisha jamii inayozunguuka hifadhi.
8. Kutoa
elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya msitu kabla na baada ya kuwaondoa
wavamizi.
9. Katika kuwaondoa
wavamizi sheria izingatiwe.
10.
Kuweka walinzi wa misitu baada ya kuwaondoa wavamizi.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe. |
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly. |
No comments:
Post a Comment