Mkurugenzi
wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television
mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE
wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea
uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi.
Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika
wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini
Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara
waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .
Zawadi
ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU
imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE
(Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR
MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo.
Mshindi
wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana
HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika
na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika
maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam
ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya
shilingi za kitanzania Million Tano
Katika
kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank
imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali
kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha
maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.
Wateja
hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja
vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika
kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na
Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.
Kampeni
hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba
katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa
muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi
mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama
Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.
Mkurugenzi
wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa
Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana
Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni
utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa
Akizungumza
na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi
hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya
amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma
bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao
mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili
kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.
Aidha
amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa
kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya
amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na
weledi wa hali ya juu.
Meneja
masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa
wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda
lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea
ukingoni
Ameongeza
kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank
hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi
mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa
wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni
nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi
lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank
Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.
No comments:
Post a Comment