Sunday, July 3, 2016

VIONGOZI WA DINI BAGAMOYO WATAKIWA KUHESHIMIANA.



Viongozi wa dini mbalimbali wilayani Bagamoyo wametakiwa kuheshimiana kila mmoja kwa imani yake, ili kuendelea kudumisha umoja, amani na mshikamano uliopo baina ya wananchi wote.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga alipokuwa akizungumza nyumbani kwake mara baada ya kumaliza kufuturu pamoja na wananchi wa wilaya yake.

Majid alisema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa kubwa katika jamii ya kuleta amani na utulivu, hivyo amewataka viongozi hao kuendelea kuhubiri amani miongoni mwa waumini wao ili Bagamoyo iendelee kubaki salama.

Aidha, aliwataka kutoa ushirikiano kwa serikali ya Rais, Dkt. John Magufuli ili kutekeleza azma ya Rais ya kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na uwajibikaji.

Kwa upande wao viongozi wa dini wilaya Bagamoyo wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuwakaribisha katika futari ya pamoja na kumuahidi kuto aushirikiano pale watakapohitajika.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majid Hemed Mwanga, jana jumamosi tarehe 02 Juni 2016, aliandaa futari ya pamoja na wananchi wa Bagamoyo ili kutekeleza ukarimu unaohitajika katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadahani.

No comments:

Post a Comment