Monday, July 25, 2016

WATUMISHI HEWA MKOA WA PWANI NI 355, WILAYA YA BAGAMOYO PEKEE NI 91.

Mkuu  wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Everist  Ndikilo alipokuwa  akizungumza wilayani  Bagamoyo kwenye kikao  kilichowajumuisha mkuu wa wilaya, Madiwani na  baadhi ya watumishi wa wilaya  ya Bagamoyo.


Mkoa wa Pwani una jumla ya watumishi hewa 355 huku wilaya ya  Bagamoyo ikiwa na watumishi hewa 91.

Hayo yamebainishwa katiika kikao cha mkuu wa mkoa wa Pwani kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambapo wilaya ya Bagamoyo imekabidhi taarifa ya watumishi hewa 91.

Akipokea Taarifa hiyo, ya wilaya ya Bagamoyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Everisti Ndikilo amesema mpaka kufikia sasa mkoa wa Pwani una watumishi hewa 355 waliobainika.

Alisema kufuatia hali hiyo vyombo vya usalama mkoani Pwani vinaendelea na uchunguzi ili kubaini nani aliyesababisha kuwepo kwa watumishi hewa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.

Mhandisi Ndikilo, aliongeza kuwa baada ya kukamilika uchunguzi watakaobainika kuhusika na kuwepo kwa watumishi hewa watachukuliwa hatua kulingana na namna walivyoshiriki, ambapo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu au za kisheria.

Awali akitoa Taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed  Mwanga, amesema wilaya ya Bagamoyo imebaini watumishi hewa 91 huku wengi kati yao ni walimu wa sekondari na Msingi.

Majid,  alisema wapo baadhi ya walimu wa sekondari na msingi  ambao wameenda masomoni bila ya ruhusa  na wanalipwa mishara kama kawaida, pia wanahesabika kuwa ni watumishi hewa.

Aidha, Mkuu wa wilaya alisema  kuwa ucheleweshaji  wa maombi yawalimu wanaotaka kwenda  kusoma  ni sababu iliyopelekea walimu kuondoka bila ya ruhusa na  hivyo kuisababishia  hasara  serikali kwa walipa watumishi mishahara bila yakuifanyia kazi.

Alisima wapo walimu kadhaa ambao walishaacha kazi  kwa ridhaa yao lakini  bado wanalipwa mishahara kama kawaida  akitolea mfano wa mwalimu mmoja  ambae ameacha kazi toka mwaka 2014 lakini bado alikuwa anaendelea kupata mshahara  mpaka lilipokuja agizo la kubaini watuymishi  hewa.

Aidha, aliongeza kuwa, katika idadi hiyo ya watumishi hewa 91,  watumishi 12  hawajulikani na wala hakuna kumbukumbu zao  zinazoonesha kwamba wao ni watumishi.
Madiwani wakimsikilizamkuu wa mkoawaPwani.
Mkuu wamkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, kulia,akipokea ripoti ya watumishi hewa kutoka  kwa  mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed  Mwanga.   
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Majid Hemed Mwanga, kulia akiwa na Katibu tawala wa wilaya, Erika liyegela wakisikiliza hutuba ya  mkuu wa mkoa.
Mkurugenzi waHalmashauriya  Bagamoyo, kulia, Azimina  Mbilinyi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya wakimsikilza mkuu wa mkoa wa  Pwani.
Watumishi namadiwani wakimsikiliza mkuu wa mkoawa  Pwani katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuuwa wilaya ya Bagamoyo.
Madiwani wa Halmashauriya Bagamoyo wakimsikilizamkuu wamkoa.
Madiwani, wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Madiwani wa Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze, pamoja na watumishi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment