Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhandisi, Ramo Makani (wa pili kulia) akikagua eneo la mpaka
katika Msitu wa Hifadhi wa Sayaka katika Kijiji cha Bugatu, Wilayani Magu, Mkoa
wa Mwanza, anayeongoza utambuzi wa mpaka huo ni Afisa Misitu na
Nyuki Wilaya ya Magu, Ayoub Mikae (wa tatu kulia). Kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Magu, Boniventure Kiswaga. Mhandisi, Makani hivi karibuni, aliahidi kwa niaba ya
Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini kwa
ajili ya kutafutiwa suluhu ya kudumu.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhandisi, Ramo Makani (wa sita kushoto) akiwa na wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Magu na baadhi ya Wananchi wa vijiji
vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka wakikagua mpaka wa hifadhi hiyo hivi. Kinachoonekana mbele yao ni Kigingi cha mpaka kinachodaiwa kusogezwa
mbele na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kumega eneo la Hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi, Ramo
Makani (kulia) akizungumza na wananchi wa vijiji vinavyozunguuka Hifadhi ya
Msitu wa Sayaka katika Kijiji cha Bugatu Wilayani Magu Mkoa wa Mwanza, hivi
karibuni Aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya
Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.
Naibu Waziri
Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Bugatu, Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza hivi karibuni wakati akikagua ramani ya
Hifadhi ya Msitu wa Sayaka kubaini maeneo ya mpaka yenye mgogoro.
Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga (kulia) akizungumza na
wananchi wa Jimbo lake katika Kijiji cha Bugatu Wilayani Magu hivi karibuni.
Mwananchi wa Kijiji cha Salama kilichopo
kandokando ya Hifadhi ya Msitu wa Sayaka Wilayani Magu, Charles Kassandiga
(kushoto) akitoa ombi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho la kupatiwa maeneo
ya kulima na kufuga kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi, Ramo Makani
(kulia).
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhandisi, Ramo Makani (kushoto) akiongoza kikao cha Kamati ya
Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Magu alipotembelea Wilayani humo hivi karibuni
kuona eneo la mgogoro katika Hifadhi ya Msitu wa Sayaka ambapo
hivi karibuni aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yote ya Hifadhi
yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.
No comments:
Post a Comment