Tuesday, July 26, 2016

DC. KINONDONI AKUSUDIA KUONDOA TATIZO LA AJIRA KATIKA WILAYA YAKE.

Mkuu wa wilaya  ya  Kinondoni, Aliy Salum Hapi, akizungumza na wananchi wa manispaa yake leo.


Na Sara Zuberi.

MKUU  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema amejidhatiti katika kuhakikisha anamaliza tatizo la ukosefu wa ajira katika wilaya hiyo baada ya kuanzisha   mpango wa kuondoa tatizo la ajira hususani kwa vijana.

Akizungumza  na watendaji wa kata,  wenyekiti wa serikali za mitaa pamoja  wajumbe wa maeneo, katika ukumbi  wa  King  Solomon uliopo  manispaa hiyo, Happy alisema amekusudia kumaliza changomoto ya ajira kwa vijana kwa lengo la kumaliza tatizo la uhalifu  analodai linachangiwa na ukosefu wa ajira.

Alisema kwa sasa ameandaa mpango ambao watendaji hao wa kata, vijiji wanatakiwa kwenda Nyumba hadi nyumba kuchukua orodha ya majina ya vijana ambao hawana ajira ili aweze kuwaunganisha na wajasiriamali,makampuni pamoja na wafanya biashara wakubwa ili waweze kuwasaidia na tatizo la ajira.

Aliwataka wananchi wote wa wilaya ya kinondoni kujitokeza kuandika majina siku tarehe 1 hadi tarehe 7 ya mwezi wa 8 mwaka huu.

Hapi alifafanua kuwa mara baada ya kumalika kuchukuliwa majina hayo  ambapo siku ya tarehe 15 ya mwenzi wa 8,wananchi hao watakaoandishwa majiana hayo watakutanishwa katika viwanja vya Posta Kijitonyama ambap siku hiyo wataunganishwa na wadau hao wa maendeleo.

Aidha, Hapi aliwasahii watendaji hao pamoja wajumbe wa kata kuweka ushirikiano katika mpango huo ili kuhakikisha wanaweza kumaliza tatizo la ajira. 

Wananchi wa manispaa ya Kinondoni  jijiniDar es Salaam wakimsikiliza mkuu wa wilaya  hiyo, Aliy Salum Hapi.

No comments:

Post a Comment