Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akionyesha Mashine ya mfano ya
Kieletroniki ya EFDs kabla ya kugawa kwa mashine tano katika wizara
zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo,
ambazo zitakuwa kwaajili ya kukusanya mapato katika wizara hizo.
MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za
Kieletroniki za EFDs tano kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kukusanya
maduhuli ya serikali kwa kutumia mashine hizo.
Hatua hiyo imetokana na agizo la Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara
zinazotoa huduma ziwe na mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na
kukuza uchumi wa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema
kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za serikali zitasaidia kutunza
kumbukumbu katika kupanga maduhuli.
“Mashine hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha
wananchi wanaopata huduma wanapata risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa
huduma wanazopata”alisema Kidata.
Aidha alisema kuwa, mashine hizo ni mashine za
kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu
za huduma ambazo wanazitoa.
Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah
Mwandumbya alisema watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia ili kuwa na ufaisi katika utekelezaji wa agizo la Rais la ukusanyaji wa mapato.
Baadhi ya wawakilishi
wa wizara mbalimbali za serikali wakiwa katika mkutano wa kukabidhiwa mashine
za Kieletroniki za EFDs jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment