Mjumbe wa Hospiatali ya Kimataifa ya Macho, Aliy Daric akisoma risala mbele ya wageni waalikwa, katika hiyo ya The International Eye Hospital iliyopo maeneo Victoria jijini Dar es Salaam. |
Waislamu na watanzania kwa ujumla wametakiwa
kujenga tabia ya kupima macho mara kwa
mara ili kuyapatia matibabu ikiwa yatagundulika
kuwa na matatizo.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam, na Amiri
wa shura ya maimamu nchini, Sheikh Musa Kundecha alipokuwa akizungumza katika
uzinduzi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho iliyopo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Kundecha ambae alikuwa mgeni rasmi, alisema Macho ni kiungo
muhimu kwa binadamu katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na
ibada ikiwemo usomaji wa Qur ani.
Alisema, waislamu wanapaswa kuwa na tabia ya
kupima magonjwa mbalimbali huku akisisitiza swala la upimaji wa macho
kwakuwa umuhimu wa macho ni mkubwa
katika kufanikisha mambo mbalimbali.
Aliongeza kuwa watu wengi wanavaa miwani bila ya kupima jambo ambalo ni
hatari kwakuwa miwani hutengenezwa kwa vipimo kulingana na nguvu ya macho ya muhusika hivyo kitendo cha kuvaa
miwani bila ya kupima ni kujiongezea matatizo.
Awali akisoma risala mbele mgeni rasmi mjumbe wa
Hospitali hiyo ya kimataifa ya Macho,
aliy Daric, alisema ujenzi wa Hospitali hiyo hapa nchini umetokana na mahitaji ya jamii, ambapo imebainika katika
nchi za Afrika kuna uhaba wa Hospitali
zinazotoa matibabu ya macho hasa ukilinganisha na ukubwa wa tatizo la Macho.
Alisema Hospitali hiyo ilianzishwa mwaka 2013 na
kuanza shughuli zake za tiba mwaka 2014 ambapo imeweza kuwatibu viongozi mbalimbali wa serikali,
masheikh na wa Taasisi mbalimbali lengo likiwa ni kutoa huduma sahihi na yenye
ubora.
Nae Mkurugenzi wa masoko katika Hospitali hiyo,
Adama Mwatima, ametoa wito kwa jamii kuitumia Hospitali hiyo ili kupata
matibabu ya Macho hasa ikizingatiwa kuwa
Hospitali hiyo ina wataalamu na vifaa vya
kisasa katika kutibu macho.
Mmoja wa watendaji wa Hospitali hiyo akiwaonesha Masheikh baadhi ya vyumba vya Hospitalihiyo. |
Baadhi ya watendaji katika Hospitali hiyo |
Rais waHospitali hiyo, Fatih Gunan akiwaeleza wageni waalikwa namna wanvyofanya kazi katika Hospitali hiyo |
Baadhi ya Madaktari katika Hospitali hiyo The International Eye Hospital iliyopo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania |
No comments:
Post a Comment