Halmashauri ya Chalinze mkoani pwani, imepokea
Madawati ya Sekondari yenye thamani ya
shilingi milioni 80, kutoka kwa Kampuni
ya Sayona Fruit chini ya mkurugenzi wake Shubashi Pateli.
Akipokea msaada huo wa meza na viti, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Sayona
Furt Shubashi Pateli kwa kusaidia madawati hayo ambayo yatagaiwa katika shule
tano na kwamba baada ya hapo hakutakuwa na upungufu wa madawati katika
Halmashauri ya Chalinze.
Aidha, aliwatakawadau mbalimbali katika
Halmashauri ya Chalinze kuunga mkono Mkakati wa Rais Magufuli wa kuhakikisha
kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bure na kwamba ili kuonesha kumuunga
mkono Rais kila mdau anapaswa kuchangia
maendeleoya shule ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya kusoimea.
Alisema kwa sasa Halmashauri Ya Chalinze tayari imekamilisha madawati na
kwamba haina upungufu wa madawati ispokuwa
ni uhaba wa vyumba vya madarasa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,
Mkurugenzi msaidizi wa kampuniya Sayona
Fruit, Aboubakari Mlawa, amesema mbali
na msaada huo kampuni yake imepanga
kutoa madawati ya shule zamsingi yapatayo 1200 yenye thamani ya milioni 90, kwa
Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo.
Nae
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa, amesema kufuatia msaada huo Halmashauri ya Chalinze imekamilisha
utengenezaji wa madawati na kwamba
kilichobaki kuyasambaza
kwenye shule zenye mahitaji hayo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo katika shule ya sekondari Lugoba, nyuma yake ni mkurugenzi msaidizi wa Sayona Fruit Abouubakari Mlawa, anaefuata mwenye suti rangi ya udongo ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa, wa pili kulia ni makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,
Waliokaa kwenye Dawati kushoto ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, kulia ni Mkurugenzi msadizi wa kampuni ya Sayona Fruit bwana Aboubakari Mlawa wakijaribu kukalia moja kati ya madawati yaliyotelewa, waliosimama kutoka kushoto ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Lugoba, Abdallaah Sakasa, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, aliyesimama kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu, (katikati) akifurahia jambo pamoja na makamo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kulia, kushoto ni mkuu wa shuleya sekondari ya Lugoba wakati wa kupokea madawati yaliyotolewa na Sayona Fruit.
Mkuu wa shule ya sekondari Lugoba Abdallaah Sakasa kushoto akimkabidhi kiloba cha Chooko Mkurugenzi msaidizi ikiwa ni zawadi kwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Sayona Group, Shubash Pateli ambae hakuwepo wakati wa tukio.
Baadhi ya madawati yaliyotolewa
No comments:
Post a Comment