Saturday, July 23, 2016

DKT. JAKAYA KIKWETE, AKABIDHI UENYEKITI WA CCM TAIFA KWA DKT. JOHN MAGUFULI, JIONI YA LEO MJINI DODOMA.


Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka mshindi kwa kura zote za ndio zipatazo 2,398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharibika.  
 
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo, kushoto, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti Mpya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulia, Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na ushindi wa kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe wote 2,398 na hakuna kura zilizoharibika.
 
Makamu Mwenyekiti-Zanzibar, Dkt Aliy Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa ccm Taifa, Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10, pichani katikati anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. 
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya, Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10 leo mjini Dodoma.
 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Benjamin William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa ccm Taifa, Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
 
Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa chama cha mapinduzi CCM, mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho leo mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment