Kiboko akiwa ndani ya mto Wami ambao umepita kwenye Hifadhi ya Wami Mbiki. |
Serikali wilayani Bagamoyo, inaandaa mkakati wa
kuinusuru hifadhi ya Wami Mbiki ambayo inashirikisha wilaya tatu za Bagamoyo,
mvomelo na Morogoro vijijini, ili kulinda misitu na wanyama waliomo ndani yake
kwa manufaa ya Taifa.
Mkakati huo umeelezwa na mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, katika ziara aliyoifanya kwenye hifadhi ya
Wami Mbiki inajumuisha wanyama na misitu.
Katika
ziara hiyo iliyowajumuisha Wakala wa Hifadhi za Misitu Tanzania TFS, na
kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo ililenga kubaini madhara
yaliyopatikana katika hifadhi hiyo ya Wami mbiki na
kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Mkuu huyo
wa wilaya alisema ili kuweza kudhibiti mipaka ya hifadhi hiyo
na kulinda maliasili zilizomo ndani yake ni muhimu kuimarisha ulinzi wa
mipaka katika vijiji vinavyozunguuka hifadhi hiyo.
Alisema wilaya
ya Bagamoyo inaandaa mkakati ambao utawashirikisha wakuu wa wilaya zote
tatu zinazozunguuka hifadhi hiyo ambazo ni Bagamoyo, Mvomelo na Morogoro
vijijini.
Aliongeza kuwa , kufuatia maliasili zilizomo ndani ya hifadhi hiyo, Taifa
linaweza kufaidika ikiwa utawekwa ulinzi
utaimarishwa na ukawekwa utaratibu mzuri wa
watu mbalimbali kutembelea hifadhi hiyo kwa kulipa kiingilo.
Meneja msaidi wa TFS wilaya ya Bagamoyo, Joel Liyangala. |
Kwa upande wake meneja msaidizi wakala wa hifdhi
za misitu Tanzania TFS, wilaya ya
Bagamoyo, Joeli Liyangala, alisema, hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto
kadhaa ikiwemo nguvu ndogo ya ulinzi ukilinganisha na ukubwa wa eneo lenyewe.
Alisema
lengo la kutembelea hifadhi hiyo
pamoja kamati ya ulinzi na usalama ni kuangalia namna ya kupanga mikakati ya ulinzi ili kudhibiti
uharibifu unaofanywa katika hifadhi hiyo ikiwemo uvunaji wa mbao
na uchomaji mkaa huku wanyama waliopo katika hifadhi hiyo wapo hatarini
kutoweka kwa kukosa ulinzi wa kutosha.
Liyangala alisema, hifadhi ya Wami Mbiki ina
wanyama wengi wanoishi humo huku wakifanya njia kuu ya kutoka mbuga mbalimbali kuelekea Seluu.
Askari wa hifadhi ya Wami Mbiki wakiwa kwenye ulinzi. |
Aliongeza kwa kusema, hifadhi ya Wami Mbiki ina
ukubwa wa hekta 2500 ambapo inajumuisha
vijiji 24 vinavyozunguuka hifadhi hiyo, kutoka katika wilaya 3 za Bagamoyo,
Mvomelo na Morogoro vijijini.
Askari wanaolinda hifadhi ya Wami Mbiki, wakimueleza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid hemed Mwanga, hayupo pichani, changamoto wanazokabiliana nazo |
No comments:
Post a Comment