Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Mh. Christina Mndeme akiwasha Mwenge wa uhuru katika mnara wa
mashujaa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ambayo inaadhimishwa leo 25 Julai, hafla iliyofanyika Saa Sita
Kamili usiku ya tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.
Mwenge wa uhuru mara baada ya kuwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mjini Mh. Christina Mndeme, Tarehe 25 julai 2016 Saa Sita Kamili usiku Mkoani
Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa
viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuupa heshima Mkoa wa
Dodoma ambapo maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo.
Wanajeshi wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge usiku wa saa sita, kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya Mashujaa yanayofanyika hii leo tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia uwashwaji wa
Mwenge katika mnara wa Mashujaa usiku wa saa sita mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali
waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kutoa rai kwa watanzania
kuwa wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya mtu kama walivyofanya wazee
wetu waliopigania uhuru wa nchi.
.................................................................................................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa kufanyika kwa
maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa inawakumbusha watanzania kuwa wazalendo.
Akizungumza wakati wa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa sambamba na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru katika mnara wa kumbukumbu za Mashujaa, leo usiku katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma, Waziri Mhagama alisema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya Mashujaa mkoani Dodoma ni heshima kwa wananchi wa Dodoma na watanzania wote kwa ujumla.
“Kufanyika kwa maombolezo haya inatukumbusha watanzania kuwa wazalendo na kupigania bila kuchoka, bila kujali makabila yetu na tujifunze kwa Mashujaa hawa waliopigania uhuru wetu” alisema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama aliwaomba watanzania kutumia siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo ni Julai 25, kwa namna mbalimbali ikiwemo kufanya maombi ya sala kwa Mashujaa wote walifariki katika harakati mbalimbali za kupigania uhuru wa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimwa Jordan Rugimbana aliishukuru Serikali kwa uwamuzi wa kuadhimisha kumbukumbu za mwaka huu za Mashujaa mkoani Dodoma, na kusema kuwa kufanyika kwa tukio hilo la kihistoria linakumbusha uwajibu wa watanzania na Mkoa wa Dodoma utaienzi heshima hiyo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme aliwasha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Mnara wa Mashujaa uliopo mkoani Dodoma ni kati ya vituo 4 vilivyopo nchi nzima ambavyo vimekuwa na makaburi ya Mashujaa mbalimbali waliopigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Vituo vingine vipo meneo ya Mtwara, Dar es Salaam na Kagera.
Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu yanafanyika leo julai 25, mkoni Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi.

No comments:
Post a Comment