Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, mwenye miwani kushoto, akiongea na viongozi wa kimasai kuhusu mikakati ya kuwapeleka watoto shule. |
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lulenge kata ya Ubena
wilayani Bagamoyo, Lukasi Sultani, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kula
njama za kutaka kumuozesha mwanafunzi wa kidato cha kwanza.
Mwenyekiti huyo wa Kitongoji, ambae piya ni
mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Bagamoyo, amekamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa raia wema waliovujisha
siri huku mwanafunzi akiwa amepatikana
kabla ya ndoa kufungwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkurugenzi wa shirikan
la kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ndoa za utotoni, ESUPAT (CHEMA) Ester Labani
Moreto, alisema mara baada ya mwanafunzi Margret Minaura kufaulu mwenyekiti
huyo alimuombea uhamisho kutoka shule ya Ubena kwenda shule ya Mikumi.
Aliongeza kuwa, mara baada ya kufuatilia katika
shule ya Mikumi iligundulika kuwa hakufika shuleni na kwamba alifichwa kwa
lengo la kuozeshwa kwa mtoto wa mwenyekiti huyo wa kabila la jamii ya wafugaji.
Ester, alisema kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya
ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, iliandaa mtego na baadae kukamatwa
mwenyekiti huyo na kumfikisha mahakani.
Aidha, alisema mwanafunzi huyo yupo chini ya
Shirika lake la ESUPAT (CHEMA) na kwamba kwa sasa anafanyiwa utaratibu wa
kupelekwa shule ili kuendelea na masomo ambapo aliwaomba wadau mbalimbali,
kusaidia shirika lake kwakuwa linakabiliwana na changamoto kadhaa katika kulea
watoto wenye mazingira magumu na wajane.
Akielezea hali hiyo, mwanafunzi aliyenusurika
kuolewa Margret Minaura, alisema yeye aliambiwa anahamishwa shule na hakutakiwa
kwenda kwenye shule aliyochaguliwa ambapo mwenyekiti huyo akishirikiana na mama mzazi wa msichana huyo, walipanga njama zakumuozesha kwa mtoto wa mwenyekiti anaetuhumiwa.
Hata hivyo, Margret, ambae ni yatima wa kufiwa na
baba yake, alisema bado anatamani kusoma na kwamba anahitaji msaada kwa wadau
mbalimbali ili aweze kuendelea na masomo.
Aidha, Margret alimshukuru mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, kwa kufanikisha kumnusuru na ndoa ya utotoni, na
kwamba amemuomba mkuu wa wilaya kuendeleza msako huo kwakuwa wapo watoto wengine ambao
wanaolewa hali ya kuwa bado ni wanafunzi shule za msingi au Sekondari hasa katika kabila wamasai.
"Yupo mwanafunzi mwenzangu tumemaliza wote darasa la saba na yeye amefaulu, lakini ameolewa, namuomba mkuu wa wilaya awanusuru wasichana wengine kama mimi ili wapate elimu" Alisema Margret.
"Yupo mwanafunzi mwenzangu tumemaliza wote darasa la saba na yeye amefaulu, lakini ameolewa, namuomba mkuu wa wilaya awanusuru wasichana wengine kama mimi ili wapate elimu" Alisema Margret.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid
Hemed Mwanga, alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wadogo
hasa wale wenye umri wa kwenda shule ili kila mtoto apate haki ya kupata Elimu
ambayo inatolewa bure.
Aliongeza kuwa msako utapita wa nyumba hadi
nyumba hasa kwa jamii wa wafugaji ambao
wanaonekana kutopenda kuwapeleka watoto shule ili kuwakamata wazazi
ambao watoto wao hawakuwapeleka shule.
Mkurugenzi wa shirika linalopinga ukatili wa kijinsia, na ndoa za utotoni, ESUPAT, Ester Labani Moreto |
Msichana aliyenusurika kuolewa hali ni mwanafunzi, Margret Minaura, ambae bado anahitaji kusoma. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, akisikiliza hoja za kina mama wa kimasai katika kitongoji cha Kivuga kata ya Ubena ambao watoto wao hawajapelekwa shule. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, akiwa na watoto wakimasai ambao hawajapelekwa shule, katika kitongoji cha Kivuga, kata ya Ubena. |
Wananchi wa jamii jamii ya kimasai wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, katika mkutano uliofanyika kijiji cha Pongwe Msungura. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, akikabidhiwa mtoto wa kimasai mara baada ya kuwatembelea katika makazi yao kitongoji cha Kivuga. |
No comments:
Post a Comment