MRADI WA BOMBA LA MAFUTA MULEBA KUKAMILIKA SEPTEMBA-TPDC

 

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo kilichopo Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda wilaya ya Muleba

................................


Na Alodia Dominick, Muleba


Mradi wa bomba la mafuta uliotarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu 

umekwama kukamilika kutokana na vipuli vinavyotoka nje ya nchi kutofika kwa wakati.


Vipuli hivyo ambavyo havikutajwa vinatoka nchi gani vimekwamisha kuanza kusukumwa kwa mafuta ambayo yalitarajiwa kuanza kusukumwa mwezi Julai mwaka huu katika kituo cha Muleba   badala yake mradi huo utakamilika rasmi mwishoni mwa mwezi Agosti au mwanzoni mwa Septemba 2026.


Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, amesema kuwa, mradi wa bomba la mafuta ulitarajiwa kukamilika rasmi mwezi Julai mwaka huu lakini kutokana na vipuli ambavyo vinapaswa kutoka nje ya nchi vimekwamisha mradi.


"Mradi wetu wa bomba la mafuta ulipaswa kukamilika rasmi Julai mwaka huu lakini kutokana na kuchelewa kwa vipuli ambavyo vinapatikana nje ya nchi vimekwamisha mradi huu badala yake utakamilika rasmi mwishoni mwa mwezi Agosti au mwanzoni mwa Septemba 2026 kwa sasa uko asilimia 88"amesema Moshi


Moshi amesema TPDC, inamiliki asilimia 15 ya hisa katika EACOP, imepata uzoefu mkubwa kupitia utekelezaji wa mradi huo, hususan katika ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.


Amesema, manufaa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) yanaendelea kuonekana mkoani Kagera, huku ujenzi wa kituo cha kusukuma Mafuta Ghafi Namba Tatu (PS3) katika Wilaya ya Muleba ukifikia asilimia 88.


Kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda wilaya ya Muleba, kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Agosti au mwanzoni mwa Septemba mwaka huu, baada ya ujenzi wake kuanza Aprili 2024.


Mradi wa EACOP unamilikiwa na Total Energies kwa asilimia 62, TPDC asilimia 15, Uganda National Oil Company (UNOC) asilimia 15 na CNOOC Limited ya China asilimia 8.


Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamesema kuwa, mradi wa bomba la mafuta ukikamilika utachochea shughuli za kiuchumi katika maeneo unapopita mradi huo.




Comments

Popular posts from this blog

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO NANENANE

SAMIA URGES FASTER INFRASTRUCTURE DELIVERY ACROSS AFRICA.

WANAFUNZI WA SHULE YA VIPAJI YA KIBAHA SEKONDARI KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA UCHAKAVU WA MADARASA

VERONICA MREMA WA TANZANIA AINGIA SITA BORA TUZO ZA ISU ELIHLE 2026 AFRIKA