MWENYEKITI WA CCM BAGAMOYO ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA MBUNGE JIMBO LA CHALINZE MAREHEMU IDDI SWALA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo Cde. Abubakar Mlawa,
ameungana na Viongozi mbalimbali wa Siasa, Serikali, Dini, Michezo, Ndugu, jamaa na mamia ya wombolezaji katika kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bagamoyo, Katibu wa Uchumi Wilaya na Katibu wa Mbunge Jimbo la Chalinze, Marehemu Iddi Said Swala nyumbani kwa marehemu Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mwili wa marehemu Iddi Said Swala umepumzishwa leo Katika Makaburi ya familia Vigwaza.
Mlawa aliwapa pole familia kwa msiba Mzito uliowapata na kuwataka wawe na uvumilivu kipindi hiki Kigumu na amewaasa waombelezaji kuendelea kushirikiana na kumuommbea marehemu Duwa ili aweze kupumzika kwa amani na Mwenyezimungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Pia aliwashukuru familia ya Marehemu Iddi Said Swala, pamoja na Wananchi wa Vigwaza, Chalinze na Bagamoyo kwa ushirikiano walioutoa wakati wa uhai wake.
Aidha Mazishi hayo yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Bagamoyo Ramadhani Lukanga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe.Subira Mgalu, Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Mhe.HAMOUD JUMAA.
Iddi Saidi Swala amefariki dunia tarehe 13 Agosti 2026 jijini Dar es salaam na mwili wake kusafirishwa hadi Vigwaza Chalinze kwaajili ya mazishi yaliyofanyika leo tarehe 14 Agosti 2026.






Comments
Post a Comment