SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.



Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Shaibu Ndemanga amefungua Mafunzo ya Jeshi la Akiba yanayofanyika  Kata ya Zinga Wilayani  Bagamoyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 61.


Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi kwa mshauri wa Jeshi la Akiba kwa kuhakikisha Mafunzo yanafanyika kila wakati licha ya kuwa na Changamoto mbalimbali zilizopo.


Pamoja na hayo pia ametoa pongezi kwa Afisa Tarafa wa Yombo pamoja na Mtendaji kata ya Zinga kwa kukubali Mafunzo hayo kufanyika Katika Kata ya Zinga pamoja na kuwapongeza wanafunzi wote waliojitokeza katika Mafunzo hayo ya jeshi la Akiba.


Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kasi ya kujengwa kwa viwanda katika Kata ya Zinga ni kubwa hivyo ni fursa kwa vijana wote ambao tayari wampata Mafunzo hayo ili kuweza kupata fursa katika viwanda hivyo.


Aidha Mhe Ndemanga ameeleza kuwa  kutokana na Fursa hizo ambazo tayari nyingine zinahitaji Vijana na kusema kuwa uongozi uone namna bora ya vijana hao kupata fursa katika sehemu hizo ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa Ajira.


Pia Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kwa dunia ya sasa uimara na Afya bora ndio Msingi, hivyo Mafunzo hayo yanafaida kubwa licha ya kuwa na fursa mbalimbali ya kupata Ajira lakini pia yanasaidia kuimarisha Afya pamoja na kuwa wazalendo katika Taifa kwa ujumla.


Vilevile Mhe Ndemanga amewataka wanafunzi hao kutunza nidhamu katika kipindi chote cha Mafunzo na baada ya mafunzo hayo na kuweka usikivu kwa wakufunzi kwa kile wanachokifundisha na kukielewa vizuri.


Mafunzo hayo ya Jeshi la Akiba kundi la 26 yameanza tarehe 7 Julai 2026 yakiwa na Jumla ya wanafunzi  61 wanawake 11 na Wanaume 50.









Comments

Popular posts from this blog

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026

SAMIA: MAULID ITUKUMBUSHE KUISHI KWA UPENDO NA AMANI

RAIS, DKT. SAMIA, ARIDHIA KUJIUZULU MAKAMU WA RAIS.

WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

LISU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU.

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.