LISU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU.
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemkuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili. Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 21 Agosti 2026 baada ya Mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka unaoongozwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), na kujiridhisha kuwa ushahidi huo unatosha kumtaka mshtakiwa kutoa utetezi wake. Akisoma uamuzi huo, Jaji Ndunguru, anayeongoza jopo la majaji linalosikiliza shauri hilo, amesema Mahakama imechambua ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na kubaini kuwa umefikia kiwango kinachomhitaji Lissu kujibu tuhuma zinazomkabili. Uamuzi huo unaashiria kuingia kwa kesi hiyo katika hatua muhimu ya utetezi, ambapo Lissu atapata fursa ya kueleza upande wake wa jambo mbele ya Mahakama. Katika hatua hiyo, upande wa utetezi utakuwa na nafasi ya kuwasilisha ushahidi wake, kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili pamoja na...











Comments
Post a Comment