KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA MADINI.

 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Subira Mgalu (Mb), wamekutana na Watendaji wa Wizara ya Madini wakiongozwa na Waziri wake. Mhe. Anthony Mavunde (Mb) Agosti 11, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Bunge.


Katika kikao hicho, Kamati imepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Madini kuhusu hali ya sekta ya madini nchini, ikijumuisha uzalishaji, biashara, masoko, uwekezaji, mauzo ya nje na makusanyo ya maduhuli ya Serikali.


Baada ya kupokea na kujadili taarifa hiyo, Wajumbe wa Kamati walitoa maoni yao ya kuboresha sekta ya madini nchini kuanzia kwenye uchimbaji, uuzwaji na masuala ya kodi yanayohusika katika biashara ya madini.







Comments

Popular posts from this blog

DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO NANENANE