BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026
Baraza Kuu la waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi Swala Allahu Alayhi Wasalam, kuwa ni siku ya jumanne ya tarehe 25 Agosti 2026.
Katika Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaji, Nuhu Jabiri Mruma, imesema Maulidi itasomwa usiku wa siku ya jumatatu ya tarehe 24 Agosti 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.



Comments
Post a Comment