ASKARI WA STPU PWANI WAASWA KUENDELEA KUTOA ELIMU, ILI KUPUNGUZA WIZI WA MIFUGO.

 

Askari wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) Mkoa wa Pwani wameaswa kuendelea kujikita katika utoaji elimu hususani katika jamii za wafugaji, hatimaye kupunguza matukio ya wizi wa mifugo Mkoani humo.


Akizungumza katika kikao kazi na Askari hao leo Agosti 14, 2026 Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Nchini (STPU) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Pasua amesema kuwa ni vyema Askari hao wakazidi kuimarisha ulinzi katika maeneo ya ufugaji mkoani humo, huku akiwataka kujikita katika utoaji wa elimu ambayo itasaidia kupunguza uhalifu.


Kamanda Pasua amesema kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa hawana uelewa juu ya faida ya  kuripoti kwa wakati matukio ya wizi wa mifugo, huku akiwataka askari hao kutoa elimu hiyo pamoja na kutoa elimu ya mazizi salama na ufugaji wa kisasa ambao utachangia kupunguza matukio ya wizi wa mifugo.


Aidha Kamanda huyo amewaagiza Maafisa wa Polisi mkoani humo, kusimamia nidhamu ya Askari wakati wote huku akiwataka askari kujitambua na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za Nchi.





Comments

Popular posts from this blog

DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

HALMASHAURI YA BAGAMOYO YATENGA SHILINGI BILIONI 2, KWA MWAKA 2026/2027.

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

BIL 31 KUKAMILISHA BARABARA YA LAMI KIBONDO MJINI