DKT. BASHIRU ALLY, AVITATKA VYAMA VYA USHIRIKA KUSAIDIA WAKULIMA.




Waziri wa mifugo na uvuvi Dkt Bashiru Ally akizindua benki ya ushirika (Coop bank) tawi la Kagera
...................................

Na Alodia Dominick, Bukoba

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt Bashiru Ally Kakurwa amevitaka vyama vya ushirika nchini kwa kushirikiana na Coop Bank kusaidia wakulima katika kuongeza thamani ya mazao yao ili waweze kujiongezea uchumi.

Dkt Kakurwa ameyasema hayo Augosti 18, 2026 wakati akizindua tawi la Benki ya ushirika (Coop Bank) mkoani Kagera ambapo amesema kuwa, mazao ya wakulima yanapaswa kuongezewa thamani ili yaweze kuwapa faida na kuongeza uchumi wao.

"Tuangalie maeneo yaliyosahaulika kwenye mnyororo wa thamani tuweke nguvu, serikali inatoa fedha kwa vijana wanaofuga na kuvua kisasa, lakini mazao yao yako kwenye hatari kwa sababu hatujawaunganisha kwenye mfumo wa kuhifadhi mazao yao, mfano hawana vifaa vya kutunza ubaridi" amesema Dkt. Kakurwa

Ameongeza kuwa, kwa vyama vya ushirika kuna fursa kwani wana magala na majumba mengi lakini hayana matumizi, maghara hayo yanaweza kutumika kuweka mazao ya mavuno na kuyarejesha katika mfumo wa mzunguko 

"Mna rachi, ardhi kubwa angalieni mwelekeo wa uchumi je una kwenda kwenye kilimo, mifugo au uvuvi, tafuteni watu binafsi wawekeze kisha nyie vyama vya ushirika muhangaike na vitu vikubwa" 

Dkt Kakurwa ameeleza kuwa, wananchi wafuge na kulima kilimo mseto wafuge kuku, ng'ombe wa maziwa, walime kahawa na kilimo cha mbogamboga ili muunganiko na sekta za uvuvi na kilimo viwe pamoja, wafuge samaki, kuku na alime mazao yote na kati ya mikoa inayoweza kilimo mseto Kagera ni mojawapo.

Ameeleza kuwa, benki ya ushirika (Coop Bank) iangalie maeneo yaliyosahaulika na yenye changamoto kubwa waongeze nguvu ili wananchi wainuke kiuchumi.

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya ushirika (Coop Benk) Godfrey Ng'urah amesema, Benki hiyo tangu imezinduliwa na Rais Samia ni mwaka mmoja na nusu ambapo wakati inazinduliwa mwaka jana kitabu cha mizania ya Benki na raslimali zilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 45 baada ya mwaka mmoja imekua na kufikia shilingi Bilioni 235.

Ng'urah amesema kuwa, mwaka jana, Benki ilikuwa na matawi matatu na sasa imezindua tawi la saba Kagera na kuwa sambamba na kufungua matawi kila mkoa watajielekeza katika shughuli za kidijital nchi nzima.

"Kufikia mwishoni mwa mwaka juzi tumetoa mikopo shilingi  bilioni 14 na nusu, ya mwaka huu ni shilingi bilioni 136 na asilimia 50 ya mikopo hii imeenda kwenye vyama vya ushirika, katika kilimo shilingi bilioni 76 zimechagiza kuongeza thamani kupata masoko kwa wakulima, zana za kilimo lakini zaidi tumesaidia vyama vikuu na vyama vya msingi, pembejeo, kupata trekta na kuhakikisha wanapata masoko ya mazao baada ya mavuno" amesema Ngu'rah

Aidha ameeleza kuwa, katika mifugo na uvuvi sh bilioni 5 zimekwenda katika  ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba jijini Mwanza na zaidi ya sh bilioni 2 zimekwenda kwenye kuongeza mazao ya maziwa na chakula.

Leonard Kachebonaho Mkurugenzi wa shirika la Kaderes linalojihusisha na kuchakata kahawa wilaya za Karagwe na Kyerwa amesema kuwa, wanapaswa kushikamana ili kuondoa umaskini.

Amesema Kaderes wanao mradi wa kopa n'gombe lipa maziwa na wananchi zaidi ya 1,700 wameishanufaika na wanayo maombi ya wananchi 1,500 hivyo kutokana na anapopata n'gombe hao katika kiwanda cha Kahama fresh ambaye amekuwa akifuata mitamba ya n'gombe nchi za Uganda, Kenya hivyo yeye ana hekali 8,000 za ardhi Buchurago benki ya ushirika ikimwezesha anaweza kufuga mitamba ya n'gombe Kahama Fresh wakawa wanapata mitamba hiyo kwake.

Dkt Bashiru Ally akisalimiana na mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahya Kido

Comments

Popular posts from this blog

HALMASHAURI YA BAGAMOYO YATENGA SHILINGI BILIONI 2, KWA MWAKA 2026/2027.

BIL 31 KUKAMILISHA BARABARA YA LAMI KIBONDO MJINI

SERIKALI YAPELEKA BIL 370 KUKARABATI RELI YA TABORA-MPANDA

KAMATI YA BUNGE (PIC) YAITAKA TANAPA KUBORESHA UWEKEZAJI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA.

KAMATI YA UCHUMI UJENZI NA MAZINGIRA BAGAMOYO YAKAGUA MIRADI.

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026

WAFANYABIASHARA WASISITIZWA KUTOA NA KUDAI RISITI HALALI

DC NICKSON SIMON: USHIRIKIANO WA SERIKALI NA NGOs NI NGUZO YA MAENDELEO YA WANANCHI