Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Mh. Subira Mgalu, ametembelea wajasiriamali, wakulima, wafugaji na wavuvi katika kilele cha maonesho ya wakulima nanenane 2026 kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.
Mgalu amewapongeza wote kwa juhudi zao za kukuza uchumi kupitia kilimo, ufugaji na uvuvi na kusema kuwa serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inaunga mkono juhudi za wakulima ndiomana imetenga fungu maalum litakalogawanywa katika sekta za kilimo,uvuvi na wafugaji.
Aidha, amewapongeza wajariamali kwa kuboresha bidhaa wanazozalisha na kuziweka kwenye muonekano wenye kuvutia ili kuingia kwenye ushindani wa kibiashara.
Amesema ubora wa bidhaa unaanzia kwenye muonekano na kwamba,ubunifu wao kuboresha muonekano unawapa hadhi ya kufikia malengo waliyojiwekea katika kupeleka mbele bidhaa zao.











No comments:
Post a Comment