Popular posts from this blog
HALMASHAURI YA BAGAMOYO YATENGA SHILINGI BILIONI 2, KWA MWAKA 2026/2027.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo Halmashauri ya mji wa Bagamoyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 2 ili kutekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani. Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema pia inatarajia kupokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni 7 kutoka Serikali kuu, huku zaidi ya milioni 474 kutoka kwa wafadhili kwaajili ya miradi mbalimbali. Amesema fedha hizo za mapato ya ndani zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali kwa mwaka wa 2026/2027 huku miongoni mwa miradi hiyo ikienda kuunga juhudi za kutekeleza Dira ya Taifa ya mwaka 2050. Alifafanua kuwa, miradi yote hiyo inalenga Kwenda kuwakwamua wananchi wakazi wa Bagamoyo katika kuboresha huduma mbalimbali na miundombinu ya mji wa Bagamoyo. Selenda alisema mwaka 2021/2022 Halmashauri ya Bagamoyo ilikuwa inatenga fedha kiasi cha shilingi Milioni mia nane 800 lakini kwa ...
BIL 31 KUKAMILISHA BARABARA YA LAMI KIBONDO MJINI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Allan Kitwe, Kibondo SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepeleka shilingi bil 31.9 kukamilisha matengenezo ya km 25.9 za barabara ya lami ambayo ni mchepuko wa barabara kuu inayoingia Kibondo Mjini. Ujenzi wa barabara hii inayoanzia eneo la Nduta Junction kupitia vijiji vya Malolegwa, Kitahana na Twabagondozi hadi Kibondo Mjini ambayo awali iliishia kwenye makutano ya barabara ya Mabamba unatarajia kukamilika Desemba 2026. Akizungumzia na Mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Edson Edward amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwa kuwa itarahisisha usafiri na usafirishaji bidhaa na mazao ya wananchi. Ametaja mazao makuu yanayolimwa katika Wilaya hiyo kuwa ni maharage, mahindi, parachichi na mihogo na kudokeza kuwa kukamilika kwake kutawezesha wakulima kufikisha mazao yao sokoni kwa haraka na kwa gharama nafuu zaidi. ‘Kukamilika kwa mradi huu unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 31.9 k...
KAMATI YA BUNGE (PIC) YAITAKA TANAPA KUBORESHA UWEKEZAJI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Agosti 13, 2026, imelielekeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeleza mikakati ya kuboresha uwekezaji katika maeneo ya Hifadhi za Taifa nchini, Kuboresha miundombinu, na kuongeza mazao mapya ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania pamoja na mapato yatokanayo na shughuli za utalii. Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Rashid A. Shangazi (Mb) katika kikao kilichofanyika Bungeni Dodoma kikiwa na lengo la kupitia na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa miradi ya uwekezaji katika Hifadhi za Taifa, uhifadhi, utalii pamoja na mikakati ya kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika kukuza uchumi wa Taifa. Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Nkoba E. Mabula, viongozi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Men...
KAMATI YA UCHUMI UJENZI NA MAZINGIRA BAGAMOYO YAKAGUA MIRADI.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Ujezi na Mazingira Mhe Amiry Sanday Mpwimbwi leo tarehe 13 Agosti 2026 ameongoza Kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi inayoendelea katika Halmashauri ya Mji Bayamoyo Mwenyekiti wa Kamati ametoa Pongezi kwa uongozi wa kiwanda cha Kamal kinachotengeneza Oil kwa uwekezaji wao katika Halmashauri ya Mji Bagamoyo na kuzalisha Ajira kwa vijana wa Bagamoyo Pia Mhe Amiry amesema kuwa changamoto ambazo zimeelezwa na uongozi wa Kamal wamezichukua na watahakikisha wanazifanyia kazi ili kuona zinatatuliwa kwa wakati ili uzalishaji usikwame. Kamati ya Uchumi pia imetembelea na kukagua Maendeleo ya kiwanda cha Sinovest investment limited kilichopo Kata ya Zinga kinachofanya uzalishaji wa nguo ambapo kiwanda hicho pia bado kinaendelea na ujenzi pamoja na ufungaji wa miundombinu kwa ajili ya uzalishaji. Mhe Mwenyekiti ametoa maagizo kwa Afisa Biashara kuhakikisha wanaendelea kusimamia Yale ambayo yanaendelea katika Kiwanda hicho na kuendelea ku...
SERIKALI YAPELEKA BIL 370 KUKARABATI RELI YA TABORA-MPANDA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Allan Kitwe, Kaliua SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa kiasi cha shilingi bilioni 379.3 kwa ajili ya kuifanyia maboresho makubwa njia ya reli ya Tabora-Mpanda ili kumaliza kero ya usafiri kwa wananchi. Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Paschal Kashenshe alipokuwa akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa waliotembelea mradi huo Alisema kuwa mradi huo wa MGS (Meter Gauge Railway) unaanzia Wilaya ya Kaliua kwenda Mpanda ukihusisha uwekaji reli mpya ya zege yenye urefu wa km 210 za njia kuu na km 8 za kupishana. ‘Lengo la mradi huu ni kuongeza uwezo wa reli kupitisha tani 18.5 za mizigo kwa ekseli moja kutoka tani 13.5 za sasa, na kuongeza mwendo kasi kutoka km 30 kwa saa hadi 70’, alieleza. Alieleza kuwa kwa sasa treni hiyo inatumia muda wa masaa 12 kutoka Tabora kwenda Mpanda na masaa 9 kutoka Kaliua hadi Mpanda lakini utakapokamilika itatumia muda mfupi sana. ‘Tayari tumekamilisha ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mata...
WAFANYABIASHARA WASISITIZWA KUTOA NA KUDAI RISITI HALALI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
13 Agosti 2026, KAGERA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera imeendelea kuwakumbusha wafanyabiashara umuhimu wa kutoa na kudai risiti halali za mashine za kielektroniki (EFD) kila wanapofanya mauzo, huku ikisisitiza kuwa matumizi ya risiti bandia ni kinyume cha sheria. Akizungumza katika zoezi la Alhamisi ya Mlipakodi, Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera, CPA Joseph Mtalemwa, amewataka wafanyabiashara kuzingatia sheria na taratibu za kodi kwa kuhakikisha wanatoa risiti halali kwa wateja wao na kudai risiti wanapofanya manunuzi. CPA Mtalemwa amesema utoaji wa risiti bandia ni kosa kisheria na umewataka wafanyabiashara kutekeleza wajibu wao wa kikodi kwa uaminifu, hatua ambayo itasaidia kuimarisha uwazi katika biashara na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Katika zoezi hilo, wafanyabiashara walipata pia fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za biashara pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu maeneo wanayoona yanahitaji kuboreshwa i...
MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMATANO TAREHE 12 AGOSTI 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
DC NICKSON SIMON: USHIRIKIANO WA SERIKALI NA NGOs NI NGUZO YA MAENDELEO YA WANANCHI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
KIBAHA – Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon, amezitaka Asasi Zisizo za Kiserikali (NGOs) wilayani humo kuimarisha ushirikiano na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuongeza tija na kuleta matokeo chanya kwa wananchi. Akifungua kikao cha mashauriano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wawakilishi wa NGOs kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, DC. Nickson alisema Serikali na NGOs zina lengo moja la kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo ni muhimu shughuli na miradi inayotekelezwa iwe na mshikamano na kuendana na vipaumbele vya taifa. Alieleza kuwa ushirikiano huo unaonekana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ambapo Serikali na NGOs zote zinatekeleza miradi ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Aliongeza kuwa hali hiyo pia ipo katika sekta za afya, mazingira, haki za binadamu pamoja na uwezeshaji wa makundi maalumu. Katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya aliainisha maeneo muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele na NGOs kwa kuzi...
BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Baraza Kuu la waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi Swala Allahu Alayhi Wasalam, kuwa ni siku ya jumanne ya tarehe 25 Agosti 2026. Katika Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaji, Nuhu Jabiri Mruma, imesema Maulidi itasomwa usiku wa siku ya jumatatu ya tarehe 24 Agosti 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

































Comments
Post a Comment