KAMATI YA UCHUMI UJENZI NA MAZINGIRA BAGAMOYO YAKAGUA MIRADI.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Ujezi na Mazingira Mhe Amiry Sanday Mpwimbwi leo tarehe 13 Agosti 2026 ameongoza Kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi inayoendelea katika Halmashauri ya Mji Bayamoyo
Mwenyekiti wa Kamati ametoa Pongezi kwa uongozi wa kiwanda cha Kamal kinachotengeneza Oil kwa uwekezaji wao katika Halmashauri ya Mji Bagamoyo na kuzalisha Ajira kwa vijana wa Bagamoyo
Pia Mhe Amiry amesema kuwa changamoto ambazo zimeelezwa na uongozi wa Kamal wamezichukua na watahakikisha wanazifanyia kazi ili kuona zinatatuliwa kwa wakati ili uzalishaji usikwame.
Kamati ya Uchumi pia imetembelea na kukagua Maendeleo ya kiwanda cha Sinovest investment limited kilichopo Kata ya Zinga kinachofanya uzalishaji wa nguo ambapo kiwanda hicho pia bado kinaendelea na ujenzi pamoja na ufungaji wa miundombinu kwa ajili ya uzalishaji.
Mhe Mwenyekiti ametoa maagizo kwa Afisa Biashara kuhakikisha wanaendelea kusimamia Yale ambayo yanaendelea katika Kiwanda hicho na kuendelea kuwatembelea na kuwashauri.
Aidha pia amesema ipo haja ya kuweka nembo ambayo inaonesha bidhaa hizo zimezalishwa sehemu gani.
Katika Hakua Nyingine Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira imetembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa fremu za Biashara Bagamoyo Plaza na kupongeza juhudi zilizofanyika pamoja na kuagiza kuongeza usimamizi katika kumaliza ujenzi huo kwa Wakati uliopangwa.
Pia Kamati imetembelea eneo lililotengwa kwajili ya Dampo lililopo Kata ya Kiromo Kitongoji cha Chamgoi na kuona eneo ambalo limepangwa kwa ajili ya kuanza mchakato wa kuchimba mashimo ya dampo ili zoezi la kuhamisha Dampo la sanzale liendelee kufika mwezi wa kumi mwaka huu.







Comments
Post a Comment