HALMASHAURI YA BAGAMOYO YATENGA SHILINGI BILIONI 2, KWA MWAKA 2026/2027.

 

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo

Halmashauri ya mji wa Bagamoyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 2 ili kutekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema pia inatarajia kupokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni 7 kutoka Serikali kuu, huku zaidi ya milioni 474 kutoka kwa wafadhili kwaajili ya miradi mbalimbali.

 

Amesema fedha hizo za mapato ya ndani zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali kwa mwaka wa 2026/2027 huku miongoni mwa miradi hiyo ikienda kuunga juhudi za kutekeleza Dira ya Taifa ya mwaka 2050.

 

Alifafanua kuwa, miradi yote hiyo inalenga Kwenda kuwakwamua wananchi wakazi wa Bagamoyo katika kuboresha huduma mbalimbali na miundombinu ya mji wa Bagamoyo.

 

Selenda alisema mwaka 2021/2022 Halmashauri ya Bagamoyo ilikuwa inatenga fedha kiasi cha shilingi Milioni mia nane 800 lakini kwa sasa wameweza kufikia kiwango cha shilingi Bilioni 2 ambazo zitapelekwa katika Kata 11 za Halmashauri ya mji wa Bagamoyo.

 

Miongoni mwa miradi itakayotekelezwa ni upande wa Afya, Elimu na masoko pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 

Akielezea matumizi ya Bilioni mbili za mapato ya ndani ni pamoja na ujenzi wa madarasa manane ya shule ya Sekondari ya Shushila Ladwa, iliyopo kata ya Mapinga ambapo kwa mara ya kwanza  unakwenda kutekelezwa Mradi wa ujenzi wa madarasa ya kisasa ya ghorofa yaliyotengewa bajeti ya shilingi milioni 250.

 

Amesema ujenzi wa madarasa ya ghorofa utasaidia kubana matumizi ya Ardhi kwani mji wa Bagamoyo unakuwa na uhitaji wa Ardhi ni mkubwa ukilinganisha na ukubwa wa Ardhi iliyopo.

Alieleza kuwa katika mabadiliko ya mfumo wa elimu nchini ifikapo mwaka 2028 kutakuwa na mapokezi ya makundi mawili yanayoingia kidato cha kwanza, kwa wale watakaomaliza darasa la saba na wale watakaoishia darasa la sita  ambao wote wanatakiwa wapate vyumba vya kusomea.

 

Kutokana na hali hiyo, Selenda amesema Halmashauri ya mji Bagamoyo imejipanga ili kuhakikisha katika kipindi hicho hakuna mwanafunzi atakaeshindwa kusoma kwasababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa au vitendea kazi.

 

Mkurugenzi huyo wa Halmashauri yam ji Bagamoyo, amesema katika fedha hizo milioni mia moja zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa Barabara za mitaa ili kila mtaa uweze kufikiwa kwa urahisi.


Comments

Popular posts from this blog

DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO NANENANE