WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA
Alodia Dominick, Bukoba, Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola ambao umeendelea kushambulia wananchi nchini Congo, watumishi wa afya mkoani Kagera wamepatiwa mafunzo ya utayari kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola ili ikitokea hapa nchini wawe na uelewa mpana. Mafunzo hayo ya utayari yamefanyika Augosti 26, 2026 katika hospital ya wilaya halmashauri ya Bukoba ambapo wamefanya tukio la utayari na wataalamu wa afya wameelezwa maswala mbalimbali ikiwemo mapokezi ya mhisiwa au mgonjwa endapo akitokea katika vituo vyao. Mafunzo ya utayari yaliyotolewa kwa wataalamu wa afya ni pamoja na jinsi ya kupokea mhisiwa wa mlipuko wa ebola na wataalamu wanapopokea mhisiwa jinsi ya kumpatia matibabu/vipimo na baada ya kutoa huduma namna ya kuvua mavazi. Baada ya kutoa mafunzo ya utayari baadhi ya wataalamu kutoka wizara ya afya na wadau wengine wa afya wamezungumza na waandishi wa habari na kueleza maelengo ya mafunzo hayo. Afisa Muuguzi w...









Comments
Post a Comment