Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Bagamoyo tarehe 18 September 2023 imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ili kuona namna inavyoendelea.
Miradi iliyotembelewa ni pomoja na Mradi wa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo, mradi wa Ujenzi wa Shule ya Msingi mpya Kiharaka, Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Chasimba na Mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari Makurunge.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Sharifu Zahoro ameridhishwa na kasi ya ujenzi ya miradi hiyo kwa hatua iliyofikiwa.
Mwenyekiti huyo amewaomba wataalamu wanaohusika katika kusimamia Miradi hiyo, kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati kama ilivyopangwa.
"Niwapongeze sana wataaamu mnaosimamia mradi hii kwa kazi nzuri mnayoifanya miradi inaenda vizuri sana ninachowaambia muendelee na kasi hii mpaka kukamilika kwake huku mkizingatia thamani ya fedha inayotumika ilingane na ubora wa Miradi husika" amesema Mhe. Zahoro
Aidha Mwenyekiti huyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zinazojenga miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamlyo, pia ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo pamoja na MKurugenzi wa Halmashauri kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea Bagamoyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi..Halima Okashi amesema wataendelea kushirikiana bega kwa bega na watumishi wa Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo na itakayokuja inafanyika kwa weledi na kukamilika ikiwa na ubora uliokusudiwa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda, Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Hassan kwa kutoa fedha zinazosaidia kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Bagamoyo,
"Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutupatia fedha nyingi zinazosaidia kujenga hii miradi ambayo leo tumetembelea na kuikagua, Serikali imetupatia takribani Bilioni 1.3 iliyowekezwa katika miradi hii.
No comments:
Post a Comment