DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

 


Na Mwandishi wetu, Bagamoyo.

Mhe. Diwani wa kata Kerege ndugu Yusuph Ngoroge Augost tarehe 10, 2026 alifanikiwa kufika ofisi za Dawasa Mapinga kujadiliana na Meneja wa Dawasa tawi la Mapinga kuhusu changamoto ya maji ya vitongoji vya Kitonga, Nyakahamba na Kilemela.


Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi mara baada ya kutoka ofisi za DAWASA Mapinga, Diwani huyo wa kata ya Kerege, Mhe. Ngoroge, amesema Kitongoji cha Kitonga kimekuwa na changamoto ya maji kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ambapo maji hayatoki kwa wakati.


Alisema Kitongoji cha Kitonga ndio kuna kituo cha Afya ambapo matumizi ya maji ni makubwa kulingana na umuhimu wake.



Mh. Diwani alifikisha kilio hicho kwa niaba ya wananchi wake ambao wamekuwa wakikosa maji kwa muda mrefu hali inayoleta usumbufu kwa wananchi wa vitongoji hivyo.


Meneja alipokea changamoto na kukubaliana na Mhe. Diwani kuwa siku ya Ijumaa Augost 14, 2026  watatembelea maeneo yote ili kuona jinsi ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.


Meneja huyo wa DAWASA alisema kazi yao ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salama kwa wakati na endapo kutakuwa na changamoto za kutokufia malengo Mamlaka itachukua hatua za haraka kurekebisha hali hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO NANENANE