MADIWANI BAGAMOYO WAAGIZA MAENEO YA SERIKALI YAPIMWE.

 

Baraza la madiwani Halmashauri ya mji Bagamoyo, limetoa agizo kwa mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuyapima maeneo yote ya serikali ili kuepuka migogoro ya kiumiliki baada ya serikali kuwekeza katika maeneo hayo.


Akisoma Taarifa ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Diwani wa kata ya Dunda Amiry Mpwimbwi, amesema kamati imetoa mapendekezo ya ununuzi na upimaji wa maeneo ya Ardhi kwaajili ya viwanja kata ya fukayosi.


Wakati wa kuchangia ripoti ya kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Madiwani walikumbusha maagizo ya muda mrefu yaliyotoleawa na baraza hilo kuhusu upimaji wa maeneo ya serikali ikiwemo viwanja vya wazi, shule za msingi na sekondari pamoja na Zahanati.


Wamesema Baraza hilo limeshatoa maagizo muda mrefu ya upimaji wa maeneo yote ya serikali lakini bado utekelezaji haujafanyika hali inayopelekea kuingiza fedha za miradi kwenye maeneo ambayo hayajapimwa kisheria na baadae kuzuka migogoro ya kiumiliki.


Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamedi Usinga, amechukua nafasi yake na kutoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, kuhakikisha maeneo yote ya serikali ambayo hayajapimwa, yapimwe haraka iwezekanavyo na taarifa ziwasilishwe kwenye vikao vya Baraza la madiwani.


Usinga amesema kila kikao cha baraza la madiwani kinapokaa ipatikane taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo itakayoonesha maeneo mangapi yamepimwa na mangapi hayajipimwa kwasababu gani, na mpango utekelezaji upoje.







Comments

Popular posts from this blog

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026

SAMIA: MAULID ITUKUMBUSHE KUISHI KWA UPENDO NA AMANI

SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

RAIS, DKT. SAMIA, ARIDHIA KUJIUZULU MAKAMU WA RAIS.

LISU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU.

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

KISARAWE YAJA NA SULUHU MAHITAJI YA BARUTI, VILIPUZI NCHINI