MATUMIZI YA INTERNET NCHINI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 6.4 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MITATTU.
Matumizi ya huduma za intaneti yamezidi kuongezeka kutoka milioni 58.9 mwezi Machi 2026 hadi kufikia milioni 62.7 mwezi Juni 2026, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 6.4.
Kwa mujibu wa ripoti ya Hali ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka iliyoishia Juni 2026, inaonesha idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika.
Ripoti hiyo imefafanua kuwa huduma ya intaneti kwa njia ya simu za mkononi inapendelewa zaidi ikiwa na jumla ya laini milioni 37.6 ikilinganishwa na huduma ya intaneti isiyohamishika.
Kuongezeka kwa utumiaji wa intaneti kunatokana na ubora wa huduma na miundombinu inayowezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa kidijiti.

Comments
Post a Comment