BAGAMOYO, KAMATI YA ELIMU, AFYA NA MAJI HUDUMA ZA JAMII YAFANYA ZIARA.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji Mhe Mwanaharusi Jarufu leo tareh 13 Agosti 2026 ameongoza wajumbe wa Kamati hiyo kufanya Ziara katika maeneo yanayotoa Huduma za Kijamii.


Mhe. Mwanaharusi Jarufu pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kuona huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo na kupatiwa maelezo kuhusu huduma hizo na utaratibu wa utoaji wa huduma hizo.


Mhe Jarufu amesema kuwa  suala la uwepo wa changamoto ya ucheleweshaji wa kutoa huduma kwa Wananchi wanaohitaji huduma hasa upande wa maabara ipo haja ya kuona ni namna gani wanabadilika na kuwa na huruma kwa Wananchi hao 


Aidha Mhe Mwenyekiti huyo wa Kamati amesisitiza kuweka utaratibu mzuri ambao utamwezesha Mgojwa ambae ameenda hospitali kupata huduma kujua utaratibu uliopo na kupokelewa kwa lugha nzuri pamoja na huduma bora kwa ujumla 


Pia Kamati ya Elimu Afya na Maji imetembelea kikundi cha Ufugaji Wanawake Mvuleni kilichopo Kata ya Kisutu kitongoji cha Mji Mpya.


Mhe Jarufu amewataka wanakikundi hao kuongeza juhudi na Usimamizi katika mradi wao huo wa ufugaji pamoja na kuanza kutafuta masoko huku akiwataka kuwa  na ushirikiano.


Vilevile Kamati ilitemblea na kukagua ujenzi wa nyumba ya Mwalimu shule ya Sekondari Matimbwa Mhe Jarufu amepongeza kwa usimamizi mzuri wa mradi pamoja na kuwataka kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo tarehe 25 Agosti 2026.


Kamati vilevile imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya Msingi Bigilo huku Kamati ikitoa maagizo ya kuongeza kasi ya ujenzi pamoja na usimamizi wa karibu wa ujenzi huo na kukamilika kwa wakati.




















Comments

Popular posts from this blog

DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

BAGAMOYO: MJI WA KIHISTORIA UNAONGOJEA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI KUPITIA BANDARI MPYA

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO NANENANE