MAKAMU WA RAIS AWASALIMU WANANCHI WA CHAMWINO

 

MAKAMU WA RAIS AWASALIMU WANANCHI WA CHAMWINO


AAHIDI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU, UTII NA UZALENDO




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa dhamana ya kuwa msaidizi namba moja na kuahidi utii, uadilifu, uzalendo na uchapaji kazi.

 

Makamu wa Rais amesema hayo, wakati akiwasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino, waliojitokeza kumpokea kwa wingi nje ya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais. Amesema ataendelea kufanya kazi ya kumsaidia Mhe.  Rais kwa uadilifu na kuwatumikia watanzania wote ili kuharakisha maendeleo.

 

Aidha Makamu wa Rais amesema ataendelea kuwawakilisha vyema vijana hapa nchini na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inazidi kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

 

Akitoa salamu zake kwa wananchi hao, Makamu wa Rais amewahakikishia kuendelea kutekeleza majukumu yake mapya kwa uadilifu, bidii na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

 

“Wana sitawazingua, na Mama sitamzingua,” amesema Ndejembi, katika ujumbe uliosisitiza dhamira yake ya kutekeleza wajibu aliopewa na kuendelea kuwa mwaminifu na mwakilishi mwema wa vijana.

 

Makamu wa Rais amewasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino ikiwa ni

jimbo alilolitumikia kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

29 Agosti 2026

Dodoma.













Comments

Popular posts from this blog

WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

RAIS DKT. SAMIA AKIWA PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS DEOGRATIUS NDEJEMBI.

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026

SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

SAMIA: MAULID ITUKUMBUSHE KUISHI KWA UPENDO NA AMANI

RAIS, DKT. SAMIA, ARIDHIA KUJIUZULU MAKAMU WA RAIS.

GLOBAL YASAFIRISHA KUNDI LINGINE LA WANAFUNZI KWENDA NJE YA NCHI.

MADIWANI BAGAMOYO WAAGIZA MAENEO YA SERIKALI YAPIMWE.