MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA

 

MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA



Alodia Dominick,


 Bukoba


Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi saba yenye thamani ya sh. milioni 900 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Mwenge wa Uhuru umewasili Manispaa ya Bukoba Augosti 31, 2026 ukitokea katika wilaya ya Muleba.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda akiwa Manispaa ya Bukoba amesisitiza wananchi kuilinda amani, umoja na mshikamano kwani pasipo amani hakuna miradi ya maendeleo inayoweza kutekelezwa.


"Ni wajibu wetu wananchi wa Taifa hili kuilinda amani ya nchi yetu chini ya kauli mbiu isemayo Tanzania ni yetu sote tushikamane kuleta maendeleo sambamba na hiyo inatukumbushwa mapambano dhidi ya rushwa, madawa ya kulevya,  mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi na mapambano dhidi ya maralia" amesema Mwang'onda


 Ameeleza kuwa, ujumbe huo unawataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu uliohasisiwa na viongozi wa nchi hii na kuenziwa na viongozi katika awamu zote kwa miaka 65 sasa.


"Ndugu wananchi kwa miaka hii nchi yetu imeendelea kusifika kimataifa kwa kuwa kusiwa cha amani na heshima kwa kuendelea kuitunza tunu hii na serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wananchi ili taifa hili liendelee kusifika katika nchi za madora huku likiendelea kulinda wananchi wake kwa kuendelea kulinda utu wao na uhuru wa kuabudu" amesema Mwang'onda


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema kuwa, mwenge wa Uhuru ukiwa wilaya ya Bukoba utatembelea katika halmashauri mbili Manispaa ya Bukoba na Bukoba mjini.


Amesema, kwa manispaa ya Bukoba Mwenge umezindua, kukagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 900.


Aidha miradi hiyo ni pamoja na kituo janja cha kusambaza maji Kabare ka Ngaiza katika shule ya msingi Ibura na sekondari ya Erasto, mradi wa nishati safi ya kupikia na club ya wapinga rushwa shule ya sekondari Kagemu, vyumba viwili vya madarasa sekondari ya Kibeta, zahanati ya Hamugembe, ofisi ya mtaa pwani, mradi wa vijana Kashai na kijana mbunifu Kashai.


Ikumbukwe kuwa, mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu zilizinduliwa Aprili 2,2026 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi katika mkoa wa Kusini Pemba na zinatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 14, 2026 mkoani Rukwa, zikiwa na kaulimbiu: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane.”







Comments

Popular posts from this blog

RAIS DKT. SAMIA AKIWA PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS DEOGRATIUS NDEJEMBI.

WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

MAKAMU WA RAIS AWASALIMU WANANCHI WA CHAMWINO

MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA

GLOBAL YASAFIRISHA KUNDI LINGINE LA WANAFUNZI KWENDA NJE YA NCHI.