Kamanda wa Polisi, mkoa wa pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa,akiwaonyesha waandishi wa habari vifaa mbalimbali vilivyokamatwa kwenye msako unaondeleo mkoani humo.
NA
MWAMVUA MWINYI, PWANI.
JESHI
la polisi mkoani Pwani ,linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuiba kompyuta
mpakato saba zenye thamani ya sh. milioni 4.2 mali ya shule ya msingi Msoga
iliyopo Chalinze wilayani Bagamoyo.
Aidha
Jeshi hilo, limewakamata watu 67 kwa tuhuma za kufanya uhalifu mbalimbali
,katika misako inayoendelea mkoani humo.
Kamanda
wa Polisi, mkoa wa pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa,
aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake, kuwa siku ya tukio watu
wasiojulikana walivunja kwenye shule hiyo na kuiba vifaa hivyo.
Alieleza,
tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baada ya tukio hilo
uongozi wa shule ulitoa taarifa polisi ambao walianza msako na walikamata watu
hao wakiwa na kompyuta tatu.
“Tunaendelea
na uchunguzi kwa watu wengine ambao watakuwa na hizo kompyuta nne zilizobakia
ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,”alisema Wankyo.
Katika
tukio lingine Said Athuman (32) Mkazi wa mkoa wa Tanga amekamatwa kwa tuhuma za
kukutwa na matairi ya pikipiki 100 na 75 ya bajaji ambayo yanadhaniwa kuwa
hayakulipiwa ushuru.
Alisema
kuwa, tukio hilo lilitokea septemba 21 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku eneo
la Round About kata ya Dunda tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda
Wankyo, alifafanua ,mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Mazda Pick Up
yenye namba T 135 DPU ambapo gari hilo lilikamatwa wakati polisi wakiwa doria
na inadhaniwa mali hizo zilipitia kwenye bandari bubu zilizopo Bagamoyo.
Pia
mkazi wa Lugoba Mtupe Abdala (45) anashikiliwa kwa tuhuma za kusafirishama mbao
ngumu 60 kwa kutumia gari lake aina ya Howo lenye namba za usajili T 693 CEH/T
672 DSK bila ya kuwa na kibali.
Hata
hivyo, Kamanda Wankyo, alisema polisi walimkamata mtuhumiwa septemba 20 eneo la
Chalinze Mzee tarafa ya Chalinze wilaya ya Kipolisi Chalinze katika msako
unaoendelea wa usiku na mchana wa kukamata wahalifu.
No comments:
Post a Comment