wa Jimbo la chalinze, Ridhiwa Kikwete, akizungumza na viongozi wa CCM kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Chalinze.
....................................
Na
Shushu Joel
MBUNGE
wa Jimbo la chalinze, Ridhiwa Kikwete amewataka wana CCM jimboni humo, kutembea
kifua mbele akisema ahadi nyingi zimetekelezwa na kwamba hayo ni matokeo ya
kuichagua CCM.
Akizungumza
katika kikao cha maelekezo ya uchaguzi kwa viongozi wa kata zote 15 za jimbo la
chalinze Kikwete alisema kuwa, serikali imefanya mambo makubwa kwa wananchi na
hivyo kufanikisha utekelezaji wa ilani kwa asilimia 93.
Chama
cha mapinduzi (CCM) kimefanya mengi katika jimbo la chalinze na wilaya ya
Bagamoyo kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, mradi wa maji, kujengwa
kwa daraja kubwa la Wami, ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya
barabara na mengine Mengi.
"Kwa
Utendaji huu wa serikali ni lazima kila kiongozi na mwanaccm atembee kifua mbele
kwa kufanikisha kutatua changamoto za wananchi" Alisema Kikwete.
Aidha
Mbunge huyo ametumia kikao hicho Cha viongozi wa matawi na Wana CCM kuwataka
wakatoe Elimu kwa wananchi kulinda miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu
kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake katibu wa tawi la Magogoni kata ya kiwangwa Msisi Safisha
amempongeza mbunge kwa kuwakumbusha viongozi wa matawi juu ya kuyatangaza
mazuri yaliyofanywa na chama hicho.
"Sisi
tulikuwa tukijua kuwa kazi ya kukisemea chama juu ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo inafanywa na viongozi wa ngazi za juu tu kumbe hata sisi wa chini
tunatakiwa kusema "Alisema Safisha.
Aidha
amempongeza mbunge kwa kuwafumbua macho na hivyo amewataka viongozi wenzake
kutumia elimu hiyo ili wananchi wengine waweze kutambua kilichotekelezwa na
serikali ya awamu ya tano.
Naye
katibu wa CCM, Mkoa wa Pwani, Ally Makoa, amemsifu mbunge wa Chalinze kwa
usimamizi na utekelezaji wa ilani katika Jimbo lake kwani kazi anazozifanya
zinaonekana.
Aidha
amewataka viongozi wa matawi na kata kuwapelekea wananchi viongozi wanaowataka
wananchi na si yule asiyetakiwa.
Pia
aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wanatakiwa kujipanga ili
kisipotee hata kitongoji kimoja.
Viongozi wa CCM kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Chalinze, wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo alipokutana nao kupeana maelekezo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Picha zote na Shushu Joel
No comments:
Post a Comment